1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa wa UN na Eu watimuliwa

26 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CgPh

KABUL

Umoja wa mataifa umeingia katika mazungumzo na serikali ya Afghanstan kujaribu kuutatua mzozo ulioibuka hivi karibuni ambao umesababisha serikali ya mjini Kabul kuwatimua maafisa wawili wa kibalozi wa Umoja wa Ulaya nchini humo.

Maafisa hao mmoja ni mfanyikazi katika Umoja wa Ulaya kutoka Ireland na mwingine ni mshauri wa masuala ya kisiasa katika Umoja wa mataifa na raia wa Uingereza.Msemaji wa Umoja wa mataifa mjini Kabul amesema mzozo huu umetokana na hali ya kutoelewana iliyojitokeza baada ya maafisa hao kutembelea eneo tete la mkoa wa kusini wa Helmand.Serikali ya Afghanstan inawashutumu maafisa hao kwa kukutana na waasi wakitaliban bila ya ridhaa yake.Msemaji wa Umoja wa mataifa amefahamisha kwamba afisa wake ataondoka nchini humo katika muda wa saa 48.Haijafahamika ni lini afisa wa Umoja wa Ulaya amepangiwa kuondoka nchini humo.