1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano Iran na Makadirio kwa mwaka 2018 Magazetini

Oumilkheir Hamidou
2 Januari 2018

Maandamano ya Iran, Uhusiano wa Marekani na Umoja wa Ulaya, na makadirio ya Umoja wa ulaya kwa mwaka 2018 ni miongoni mwa mada zilizomulikwa katika toleo la mwanzo magazetini kwa mwaka mpya wa 2018.

https://p.dw.com/p/2qCzJ
Silvester 2018 in Berlin
Picha: Getty Images/A. Berry

Tunaanzia Iran ambako kilio cha vijana kimehanikiza katika miji kadhaa ya mikoani. Vijana wanasema wanataka maisha bora. Gazeti la Badische Zeitung linaandika: "Kizazi kipya ambacho muasisi wa Jamhuri ya kiislamu wanamjua kwa jina tu, wanadai wapatiwe uhuru wanaovijunia vijana wenzao katika nchi nyenginezo pamoja na kufaidika na utajiri wa nchi yao ambao kwa miongo kadhaa unawanufaisha mamullah wala rushwa na kundi la viongozi wanaotumia vibaya jina la Mungu. Kwasababau hata ufanisi wa siasa ya nje uliofikiwa na rais Rohani kwa kutia saini makubaliano ya mradi wa nuklea, natija yake bado haijawafikia wananchi wa kawaida. Uongozi wa Jamhuri ya Kiislamu unaanza kulega lega. Lakini pengine wimbi hili la malalamiko, sawa na lile la mwaka 2009 likasalia kuwa mbio za sakafuni tu katika jamhuri ya kiislam ya Iran."

Wakati wa mageuzi umewadia anasema Donald Trump

Rais wa Marekani anasema maandamano ya Iran yanaashiria mageuzi. Gazeti la "Donaukurier" linaandika: "Mwaka mpya ndio kwanza umeanza, lakini rais wa Marekani Donald Trump hajabadilika."Wakati wa mabadiliko umewadia", amesema rais huyo wa Marekani kupitia mtandao wa kijamii Twitter akishangiria maandamano yanayoendelea Iran. Kaula na chuwa! Kama kuna mafunzo yoyote yaliyotokana na balaa la Afghanistan, Iraq na Libya basi ni haya: Ni makosa makubwa kuamini kwamba baada ya kupinduliwa utawala wa zamani, amani na uhuru vitafuata moja kwa moja."

Mwaka 2018 huenda ukambadilisha Trump

Donald Trump na makadirio kwa mwaka mpya 2018 ni mada iliyochambuliwa na gazeti la kaskazini mwa Ujerumani  "Hannoversche Allgemeine" linahisi kuna kitakachobadilika baada ya uchaguzi wa nusu mhula nchini Marekani. Gazeti linaandika: "Uhusiano kati ya wamarekani na wazungu wa Umoja wa ulaya haujawahi kuwa tete kama baada ya kuchaguliwa Donald Trump kua rais wa Marekani. Lakini mwaka huu mpya unaweza kuleta mabadiliko. Watu wasishangae, kumuona Trump akidhoofika mwaka 2018 na umoja wa ulaya kuimarika zaidi kuliko wakati wowote ule mwengine. Katika uchaguzu wa nusu mhula nchini Marekani, November sita inayokuja, wanachama kadhaa wa baraza la wawakilishi na wale wa baraza la seneti watabidi wakatafute imani ya wapiga kura. Pindi mizani ikibadilika na kuelemea upande wa wademokrats katika baraza la wawakilishi, nguv u za Trump zitapungua. Na zaidi ya hayo anaweza kukabiliwa na utaratibu wa kumpokonya madaraka.Yote hayo yatamlazimisha abadilishe mtindo wake.

Mwaka 2018 utakuwa na tija pia kwa Umoja wa Ulaya

Makadirio mema ya mwaka 2018 kwa Umoja wa Ulaya yameashiriwa pia na mhariri wa gazeti la kusini mwa Ujerumani "Stuttgarter Nachrichten.

Mwandishi:Oummilkheir Hamidou/Inlandspresse

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman