1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano Iran

Thelma Mwadzaya16 Juni 2009

Waandamanaji nchini Iran wametoa wito wa maandamano zaidi kufanyika ili kuupinga ushindi wa Rais Mahmoud Ahmedinejad katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/IAQR
Waandamanaji mjini TeheranPicha: Hadi Fatemi
Iran Wahlen 2009
Hossein Mousavi na mkewePicha: MEHR

Kulingana na mpinzani wake mkuu Hossein Mousavi kura ziliibiwa katika uchaguzi huo wa rais uliofanyika Ijumaa iliyopita.Wapiganaji walio na msimamo mkali wanaoiunga mkono serikali walimuua mtu mmoja wakati wa maandamano yaliyowashirikisha maelfu ya watu hapo jana.Rais wa Marekani Barack Obama alisisitiza kuwa hataki kamwe kuuingilia uchaguzi huo ila anatiwa shaka na hali iliyoko Iran kwa sasa.