1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano makubwa yafanyika kupinga Uvamizi wa Marekani ,Iraq

Charles Mwebeya19 Machi 2007

Ikitimia miaka minne hapo kesho toka Marekani ilipoivamia Iraq kijeshi,..Maandamano makubwa yanaendelea katika miji mbalimbali duniani kupinga hatua hiyo.

https://p.dw.com/p/CB5D

siku ya pili maelfu ya watu duniani wanaendelea na maandamano makubwa kupinga hatua ya Marekani kuivamia Iraq kijeshi mnamo mwaka 2003.

Huko nchini Marekani kwenyewe mikutano mikubwa inaendelea kufanyika katika miji ya New York , Sa Francisco, Portland na miji mingine .

Toka Marekani iivamie Iraq kijeshi miaka minne iliyopita idadi ya wanajeshi 3,200 wa Marekani wameuawa .

Wengi wa waandamanaji huko Marekani walitoa mwito kwa wanajeshi walioko nchini Irak kurejea nyumbani haraka huku wakionyeshwa kukosa imani na utawala wa Rais George Bush.

Mjini New York , waandamanaji walionekana wakibeba mabango yaliyosomeka "Miaka minne ni Mingi" na maneno kadhaa yaliyoonekana kupinga uvamizi wa Marekani huko Iraq.

Leslie Kielson mmoja wa watu walioandaa maandamano hayo amesema serikali ya Rais Bush lazima ihakikishe inayarejesha nyumabni majeshi yake hivi sasa na kuhakikisha inamaliza vita huko Iraq.

Lakini kwa upande mwingine huko Los Angels waandamanaji wakiwa na bendera za Marekani walisema wanaunga mkono majeshi ya Marekani kuendelea kubaki nchini Iraq.

Mwanafunzi mmoja Leigh Wolf alisema ni muhimu kuhakikisha kuwa gharama ilizoingia Marekani zinakuwa na thamani na kwamba hiyo bado ni vita Marekani inaweza kushinda.

Vile vile maandamano hayo yalisambaa katika mji wa Portland hukufu ya waandamanaji walionekana wakikusanyika katikati ya mji huo.

Msemaji wa Rais Bush Blair Jones akiwa katika mapumziko huko Camp David aliunga mkono mipango ya serikali huko Iraq na kusema wanajeshi wa Marekani wanapigania haki na uhuru wa raia wa Iraq.

Maandamano kama hayo yalianza jana nchini Austalia na baadhi ya miji nchini Hispania.

Wakati hayo yakiendelea Bunge la Marekani wiki hii linatazamiwa kuamua kama kuna haja ya kurudisha majeshi yake kutoka nchini Iraq mapema zaidi kabla ya tarehe ya mwisho , September mosi mwakani.

Pamoja na masuala mengine , Bunge litaangalia matumizi ya vita ya Iraq.

Lakini mshauri wa masuala ya ulinzi wa Ikulu ya Marekani Stephen Hadley , katika mahojiano na Televisheni ya CNN hapo juzi , amesema endapo Bunge litaamua kuyaondosha Majeshi ya mapema zaidi ya muda uliopangwa basi kuna hatari ya Iraq kuangukia mikononi mwa Al Qaida.

Juu ya tathimini ya sera mpya ya Marekani huko Iraq, Waziri wa ulinzi Robert Gates amesema ni mapema mno kuweza kujua kama ina ufanisi kwa sasa.

Katika mpango huo mpya , Marekani ilipendekeza kuongeza vikosi vya askari wake mpaka kufikia 25,000.

Hatua hiyo ilifikiwa na Marekani kutokana na machafuko yanayoendelea kupoteza maelfu ya watu nchini Iraq.

Huu ni mwaka wa nne toka Marekani ilipoivamia Iraq kijeshi na kuuondoa utawala wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Marehemu Saddam Hussein , kwa kumtuhumu kuwa na silaha za maangamizi na kujihusisha na vitendo vya kigaidi.