1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano Urusi na Mabadiliko ya tabianchi Magazetini

Oumilkheir Hamidou
12 Agosti 2019

Maandamano ya vijana nchini Urusi, mabadiliko ya tabianchi na hatima ya mchango wa walipakodi wa Ujerumani kwaajili ya ujenzi wa Ujerumani Mashariki au Solidarpakt ni miongoni mwa mada magazetini.

https://p.dw.com/p/3NlSz
Russland Moskau Verhaftung bei Protesten
Picha: AFP/V. Maximov

Tunaanza na vuguvugu la maandamano nchini Urusi mnamo wakati huu ambapo rais wa nchi hiyo Vladimir Putin anaadhimisha miaka 20 tangu alipoingia madarakani. Gazeti la "Badische Zeitung" linaandika:"Madaraka", kama yanavyotajwa nchini Urusi, hayana hila linaapozuka suala wakabiliane vipi na kero za wananchi. Katika mji mkuu Moscow, wapinzani wanaandamana dhidi ya kutolewa mgombea wao katika orodha ya wagombea wa uchaguzi wa majimbo ambao hauna umuhimu mkubwa. Kwengineko "wananchi wa kawaida" wanaandamana dhidi ya kutupwa takataka ovyo ovyo au dhidi ya ujenzi wa njia kuu. Mageuzi ya hivi karibuni na mfumo wa malipo ya uzeeni na kodi ya mapato yamezusha hasira miongoni mwa wananchi ambazo sio tu zimemgharimu umashuhrrui wake rais Poutin bali pia  zimepelekea watu kujiuliza Putin analenga kuiongoza wapi nchi hiyo baada ya miaka 20 madarakani?"

Hakuna anaetaka kujibebesha dhamana ya mabadiliko ya tabianchi

Mjadala kuhusu mabadiliko ya tabianchi na madhara yake katika maisha ya kila siku ya jamii nao pia umepamba moto. Gazeti la "Heilbronner Stimme" linaanadika:"Madhara ya mabadiliko ya tabianchi ni ya jumla na Ulaya haitoweza kupambana nao peke yake. Ndio maana tunahitaji sera jumla ya mazingira mfano wa Umoja wa Mataifa unaoshughulikia mazingira. Na unahitajika haraka pamoja pia na kukabidhiwa nguvu muhimu za kisiasa."

 Gazeti la "Frankenpost" linashauri jinsi ya kuyahifadhi mazingira na kuandika:"Anaetaka kuyanusu mazingira anabidi aachane mara moja na garai yake na kukivunja kinu cha kupashia nyumba moto msimu wa baridi. Makaa ya mawe pia hatakiwi kuyawasha moto. Mpaka sasa mambo yanaendelea kama kawaida; Watu wanatupiana lawama; wenye kujivunia maisha ya raha hawako tayari kuachana na mtindo wao wa maisha. Hatokosa kutafuta makosa kwengineko ili mradi yeye binafsi anahakikisha halaumiwi."Inasikitisha" amenukuliwa mwanaharakati kijana Greta Thunberg" akisema alipotembelea mgodi wa makaa ya mawe wa Hombacher hivi karibuni."

Malipo ya mshikamano Solidarpakt yakurubia kumalizika

Mada yetu ya mwisho magazetini inahusu mpango wa waziri wa fedha wa serikali kuu, Olaf Scholz wa kusitisha malipo ya mshikamano au Solidarpakt. Gazeti la "Reutlinger General-Anzeiger" linaandika:"Pendekezo la Scholz ni mbinu. Kwasababau mpango wa malipo ya mshikamano utakapokamilika mwaka  2020 fedha zitakazotokana na mpango huo hazitatumiwa tena kujenga maeneo ya Ujerumani Mashariki, kwa hivyo utabidi usite. Lakini SPD hawataki kuachana moja kwa moja na mpango huo. Badala yake wanataka fedha zitakazokusanywa ziwekezwe katika sekta ya elimu na  mabadiliko ya tabianchi. Suala watu wanalojiuliza hapo ni kama dhamiri hiyo inatekelezeka kisheria.

 

Mwandishi:Hamiddou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Sekione Kitojo