1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya Urusi magazetini

13 Juni 2012

Maandamano ya upande wa upinzani nchini Urusi, hali nchini Syria na mgogoro wa fedha katika kanda ya Euro ni miongoni mwa mada zilizohanikiza magazetini hii leo.

https://p.dw.com/p/15DE4
Maandamano mjini MoscowPicha: picture-alliance/dpa

.Tunaanzia lakini nchini Urusi ambako sauti zinaziodi kupazwa kudai mageuzi. Gazeti la "Handelsblatt" la mjini Düsseldorf linaandika:Upande wa upinzani nchini Urusi umemtumia risala bayana rais Vladimir Putin. Hawatishiki. Jana waliteremka kwa maelfu majiani mjini Moscow na kudai kwa mara nyengine tena "Urusi bila ya Putin. "Wateja wengi wa kigeni wanahofia, lakini kuwepo Urusi bila ya Putin.Tangu miaka kumi na miwili iliyopita, kiongozi huyo wa zamani wa idara ya upelelezi ndiye anaedhibiti hatamu za uongozi nchini humo. Ameijenga upya nchi hiyo baada ya kipindi cha mizozo katika miaka ya 90 na kuleta utulivu.Sera zake ndizo za kushukuriwa kwamba wateja wengi kwa miaka sasa wamekuwa wakifanya biashara nono na Urusi.Wanavumilia vizingiti wanavyowekewa wananchi katika haki zao za kimsingi. Kauli mbiu ni: ukuaji bwa kiuchumi unahitaji utulivu. Putin analeta utulivu.Kwa hivyo, Putin ndie anaefaa katika kuiimarisha uchumi.

Gazeti la Delmenhorster Kreisblatt", lakini, lina maoni tofauti na hayo na linahisi:Maandamano ya maelfu ya watu yanaonyesha kwamba warusi wengi hawako tena tayari kuufumba mdomo. Hata kama maandamano hayo yametuwama kwa sehemu kubwa mjini Moscow, lakini kuanzia sasa uti wa mgogo wa kiongozi huo mwenye nguvu umeanza kudhoofika. Hata kama, kiuchumi, Urusi ina nawiri, dola hilo kuu bado linakabwa na rushwa na katika maeneo mengine ya nchi hiyo bado hakuna ishara za maendeleo zilizochomoza. Pindi Putin akiendelea kukandamiza badala ya kuleta mageuzi, basi atakuwa anazidi kunyunyizia mafuta katika cheche za moto, na kwa namna hiyo kuzidi kuwapa nguvu wapinzani nchini humo.

Symbolbild Syrien - Syriens Armee missbraucht Kinder als Schutzschilde
Mtoto atumiwa kama ngao nchini SyriaPicha: dapd

Mzozo wa Syria umemurikwa kwa mara nyengine tena na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo. Wiesbadener Kurier linauzinduwa ulimwengu kutokana na ripoti jinsi watoto wanavyoteteswa.Gazeti linaendelea kuandika:"Pindi kilio na laana za walimwengu zingesikika, basi matokeo yake yanagekuwa hujuma za kijeshi dhidi ya utawala wa Assad. Lakini kilio kimekwama rohoni kwasababu ya ripoti za kutisha kuhusu mateso na jinsi watoto wanavyotumiwa kama ngao .Hata hivyo, hujuma za kijeshi si ufumbuzi nchini Syria.Kwasababu hata kama lengo lake lingefikiwa, wahanga wasingefaidika na lolote-ushahidi umebainika nchini Libya. Huko ingawa Gaddafi ameshatoweka, lakini nchi hiyo inazongwa na vurugu. Zaidi ya hayo Libya haikuwa katika eneo tete mfano wa Syria ambayo majirani zake, si wengine isipokuwa Israel, Libnan, Iraq na Jordan.

Eurokrise Spanien Symbolbild
Mgogoro wa fedha HispaniaPicha: picture-alliance/dpa

Na ripoti yetu ya mwisho inaturejesha hapa hapa Ulaya ambako gazeti la "Donaukurier linamulika mgogoro wa fedha katika kanda ya Euro.Kuvuta wakati ndio kauli mbiu.Kuvuta wakati ili angalao kusawazisha makosa yaliyofanyika katika Umoja wa sarafu na kuyahakikishia masoko ya hisa, Ulaya inaweza kwa kila hali kuihami sarafu yake.

.......

Mwanadishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Miraji Othman