1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano yazidi Libya

22 Februari 2011

Kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi amejitokeza katika televisheni ya taifa,amekukanusha uvumi kuwa amekimbilia Venezuela.Ubalozi wa Libya katika umoja wa mataifa umelitaka jeshi kuuangusha utawala wa Gadhafi

https://p.dw.com/p/10LYe
Kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi asema hajaikimbia nchiPicha: AP

Kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi amejitokeza katika televisheni ya taifa usiku wa leo, na kwa mujibu wa televisheni hiyo ya taifa , alikuwa anazungumza nje ya nyumba yake mjini Tripoli, akikanusha uvumi kuwa amekimbilia nchini Venezuela. Mapema jana Jumatatu , hali ya mbinyo ilikuwa inaongezeka dhidi yake kumtaka ajiuzulu. Ubalozi wa Libya katika umoja wa mataifa umelitaka jeshi la nchi hiyo kusaidia kumwangusha Muammar Gadhafi. Kwa mujibu wa ripoti mbili za televisheni, kundi la maafisa wa jeshi la Libya limetoa taarifa likiwahimiza wanajeshi wengine kujiunga na umma wa nchi hiyo, na kusaidia kumuondoa kanali Gadhafi. Katika mji mkuu Tripoli, waandamanaji walipambana na majeshi ya usalama jana Jumatatu, baada ya serikali kutangaza nia ya kutaka kukandamiza maandamano. Kwa mujibu wa watu walioshuhudia , ndege za kijeshi zilishambulia makundi ya watu. Mapambano pia yametokea katika mji wa pili wa Libya Benghazi.