1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maarifa ni Nguvu

Mohamed Dahman6 Juni 2012

Elimu ni zaidi ya kupata maarifa, inamwezesha mtu kujiendeleza na kujishughulisha kwenye siasa.

https://p.dw.com/p/14oX2
Art students from the University of Helwan decorate the walls of the arts academy with murals commemorating the revolution that overthrew Hosni Mubarak in the Zamalek neighborhood of Cairo, Egypt, Wednesday, March 30, 2011. They painted icons of the protests that began Jan. 25, including Facebook, which activists used to organize protests, and symbols of Muslim-Christian unity. (Foto:Manoocher Deghati/AP/dapd)
Wanafunzi wa kike wa Chuo kikuu cha Helwan wakizipamba kuta na picha zinazokumbusha mapinduzi ya mwaka 2011 yaliyomwangusha Hosni Mubarak mjini Cairo, Misri.Picha: AP

Maarifa ni Nguvu ni hoja ilioko duniani kwa karne nne sasa. Mwanafalsafa wa Uingereza Francis Bacon ameiweka hoja hii na tasnifu nyengine kama msingi wa kuelimisha. Tasnifu yake hiyo haikupoteza uhalisi na maana yake. Imekuwa ikiyakinishwa duniani kila siku kwamba elimu ni mahitaji ya msingi kwa maendeleo ya kiuchumi na kisiasa, kwa demokrasia na kwa haki za kijamii. Hususan hilo limethibitishwa hivi karibuni wakati wa maandamano ya kupinga serikali na vuguvugu la mageuzi katika nchi za Kiarabu lilioanzia na Mapinduzi ya Asumini mwaka mmoja na nusu uliopita nchini Tunisia.

Wakati washindwa wanapokuwa washindi: Vuguvugu la maandamano ya Waarabu

Walikuwa ni wasomi na watu wa tabaka la kati walioandaa maandamano hayo. Hususan vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 35, ni wanafunzi na wanataaluma waliokuwa wamedanganywa na serikali kwa kunyimwa fursa zao. Kuanzia Rabat hadi Riadh madaktari, waandishi wa habari, wahandisi walipambana kudai uhuru zaidi, kushirikishwa zaidi, kupatiwa nafasi kwa kuzingatia haki kwenye soko la ajira na hasa kuwepo kwa muelekeo unaozingatia hali halisi ya mambo. Hawakushinda kikamilifu mapambano hayo na inabidi hivi sasa wapiganie masuala ya uchaguzi na kuimarishwa kwa taasisi za demokrasia.

Arabische Flaggenläufer mit der "Flamme der Freiheit": in der Reihenfolge der Revolutionen rennen Tunesien, Ägypten und vorne Libyen mit der Flamme auf sich entgegen streckende Hände zu; diese Hände stammen nach der Beschriftung auf den Ärmeln aus Syrien und Jemen, aufgenommen am 16.03.2012. Kurz nach Beendigung der Kampfhandlungen in Libyen entstanden in Tripolis und anderen Städten des Landes zahlreiche Wandmalereien und Karikaturen. Meistenteils zeigen sie libysche Freiheitshelden oder aber sie sollen den ehemaligen Diktator Moammar Al Gaddafi lächerlich machen oder ihn verunglimpfen. Dabei sind sie oftmals durchaus anspruchsvolle Kunstwerke. Schade nur, dass viele Mauern und Wände von den Eigentümern wieder überpinselt werden, somit sind diese Werke meistens nur von kurzer Dauer. Foto: Matthias Tödt Arabischer Frühling (arabisch ‏الربيع العربي‎, DMG ar-Rabīʿ al-ʿArabī) oder auch Arabellion[1] bezeichnet eine im Dezember 2010 beginnende Serie von Protesten, Aufständen und Revolutionen in der arabischen Welt, welche sich, ausgehend von der Revolution in Tunesien, in etlichen Staaten im Nahen Osten (Maschrek/Arabische Halbinsel) und in Nordafrika (Maghreb) gegen die dort autoritär herrschenden Regime und die politischen und sozialen Strukturen dieser Länder richten.[2]
Baada ya mapigano nchini Libya picha nyingi zilichorwa kwenye kuta za nyumba kama picha hii inayoonyesha wakimbiaji waarabu walioshika bendera na „mwenge wa uhuru“.Picha: picture-alliance/dpa

Elimu huwezesha, elimu hutoa ushiriki zaidi yumkini haya ni mambo ambayo watawala wa Kiarabu waliyadharao. Vuguvugu hilo kamwe lisingeliweza kutokea kama sio kuwepo kwa dhamira miaka 20 iliopita ya kujengwa kwa shule na vyuo vikuu katika nchi za Kiarabu. Ripoti ya Maendeleo ya Binaadamu imeonyesha kwamba nchi za Kiarabu karne mbili zilizopita zilianza kujenga elimu kwa uthabiti na kwa mafanikio ya wazi. Rais wa zamani wa Tunisia Ben Ali pia alikuwa mwanamageuzi katika masuala ya elimu.I dadi kubwa ya watu iliokuwa ikizidi kuongezeka imeelimika lakini elimu hiyo haikuwasaidia kwani kulikuwa hakuna ajira, hawakupata fursa na hawakushirikishwa. Daima vitu hivyo vilikuwa vikigawiwa miongoni mwa koo. Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Tunisia kilikuwa asilimia 40 kabla ya kuanza kwa vuguvugu la maandamano kudai mageuzi. Madikteta kama Ben Ali wangelijuwa athari ya matokeo ya kuipa elimu uzito huo wasingelifanya hivyo.

Elimu ni haki ya msingi ya binaadamu

Hakuna maendeleo bila ya elimu- hilo limekuwa likitambulika kwa muda mrefu na jamii duniani kwa ajili hiyo ndio maana zimetolewa ahadi za wazi za kisiasa.

Lengo nambari mbili la Maendeleo ya Milinia ya Umoja wa Mataifa linataka watu wote duniani wapatiwe elimu ya msingi. Hatua za maendeleo juu ya suala hilo zinapatikana lakini inachukuwa muda mrefu kuzikia na hazifanani baina ya kanda moja na nyengine. Kiwango cha watoto wanaokwenda shule za msingi kimeongezeka kwa asilimia saba tu ya kati ya mwaka 1999 na mwaka 2009 na kuwa asilimia 89.

Katika kipindi cha hivi karibuni kasi ya maendeleo imekuwa ikipunguwa. Katika nchi nyingi za Afrika na Asia lengo hilo la watu wote kuwa na elimu ya msingi ifikapo mwaka 2015 halitoweza kufikiwa. Katika nchi zinazoendelea watoto 87 kati ya 100 wanahudhuria shule ya msingi moja kwa moja. Katika nchi nyigi za kimaskini watoto wanne kati ya kumi wanaacha shule ya msingi kabla ya kumaliza shule. Wakati watoto katika vijiji na sehemu zenye migogoro wana nafasi ndogo zaidi ya kupata elimu na hasa wasichana takriban kila mahala duniani wamekuwa wakinyimwa fursa za kujiendeleza. Bado hatua zaidi zinahitajika kuchukuliwa kurekebisha hali hiyo.

Bila ya Elimu hakuna Maendeleo kwa Binaadamu

Hata hivyo katika mataifa makubwa yanayoinukia kiuchumi barani Asia kama vile India na China elimu imekuwa ikitumika zaidi kujenga uchumi. Korea Kusini katika miaka ya 1950 ilikuwa katika hali mbaya zaidi kuliko hata ile inayoshuhudiwa hivi sasa katika nchi nyingi za Kiafrika. Kuwekeza katika elimu kwa kiwango sawa kati ya wanaume na wanawake sanjari na kuboresha huduma za afya na kupatiwa madawa ya kuzuwiya mimba kumepunguza kiwango cha uzazi na kuchangia kukuza uchumi wao. Inajidhihirisha kwamba kukuwa haraka kwa uchumi wa China pia kunatokana na kiu ya elimu. Elimu ni mada kuu kwa takriban kila Mchina mwenye umri usiopindukia miaka 25 na ndio yenye kuwaamulia maisha vijana. China pia ni mfano wa serikali ambazo bado zinatowa elimu zaidi lakini bila ya kutowa uhuru zaidi. Hata hivyo taratibu hizi zitaendelea tu kufanya kazi kwa kadri zitakapokuwa zinaungwa mkono na idadi kubwa ya watu.

Ein Junge lernt im Schulunterricht den Umgang mit Computern. Foto aus der Privatschule "South Ocean International School" in Qingdao in der chinesischen Provinz Shandong, aufgenommen im Juli 2001.
Mvulana huyu wa shule ya kibinafsi "South Ocean International School" ya Qingdao nchini China anajifunza matumizi ya kompyuta.Picha: picture-alliance/dpa

Uhuru wa Kushirikishwa na kutoa Maoni

Hakuna utawala wowote halali utakaoweza kupambana na nguvu kuu zitakazojitokeza kutoka kwa idadi kubwa ya umma wa wasomi. Nguvu hizi ndizo zenye kutowa fursa za mabadiliko ya demokrasia, kwa ushirikiswaji zaidi pamoja na kushiriki kwa pamoja kwa makundi ya kijamii, kwa mfano katika nchi kama Urusi au angalau China ni kule kuanza kwa maadamano yasioendelezwa na pia katika nchi za ulimwengu wa Kiarabu.

Lakini jambo hilo inaonekana litakuwa gumu zaidi kwa nchi kama Zimbabwe, Afghanistan au Korea Kaskazini. Kwa kadri idadi kubwa ya watu itakapoendelea kuishi kwenye dimbwi la umaskini na kuzungukwa na propaganda za serikali na kwa kadri watu hao watakapokuwa hawana elimu ya kutosha kwa kulinganisha na wale wenye elimu na wala hawawezi kupata habari huru kwamba hawawasiliani kimtandao kuweza kubadilishana habari, kwa muda huo madikteta na madhalimu wanaweza kutamba na kijisikia salama. Ni hoja nzuri isiokuwa na mjadala katika kupigania haki ya msingi ya kujipatia elimu.

Mwandish: Schaeffer,Ute/ Mohamed Dahman

Mhariri: Abdul-Rahman, Mohammed