1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabaki ya ndege iliyomchukua Sala yapatikana

Sekione Kitojo
4 Februari 2019

Mabaki ya ndege  iliyomchukua  mchezaji  wa  Cardiff  Emiliano Sala  na  kupotea yapatikana,

https://p.dw.com/p/3ChSl
Artgentinien Emiliano Sala das Flugzeugwrack unter Wasser
Picha: Reuters/AAIB

Mabaki  ya  ndege  iliyomchukua  mchezaji  kutoka  Argentina Emiliano Sala  na  rubani  wake  yamepatikana  wiki  mbili  baada  ya ndege  hiyo  kupotea  katika  eneo  la  ujia  wa  maji   kati  ya Uingereza  na  Ulaya  bara, mmoja  kati  ya  wachunguzi  amesema leo.

Großbritannien FA Cup | Swansea City vs. Gillingham | Blumen für Emiliano Sala
Picha ya mchezaji Emiliano Sala akikumbukwa na mashabiki wa kandandaPicha: Getty Images/S. Forster

Sala  mwenye  umri  wa  miaka  28, alikuwa  akitokea  Ufaransa kwenda  kujiunga  na  klabu  yake  mpya, ya  ligi  ya  Premier  ya Uingereza  ya  Cardiff City, wakati  ndege  hiyo  ndogo  ilipopotea Januari 21  kaskazini  mwa  kisiwa  cha  Guernsey. Mtafutaji  wa mabaki  ya  meli  baharini David Mearns , ambaye  alikodiwa  na familia  ya  mshambuliaji  huyo baada  ya  juhudi   rasmi  za  uokozi kuamua  kuachana  na  juhudi  hizo , alisema  ndege  hiyo  ilipatikana Jumapili  asubuhi.

Premier League - Cardiff City Stadion Trauer Sala
Mbele ya uwanja wa Cardiff City kuliwekwa maua kwa ajili ya kumbukumbu ya mchezaji ambaye alikuwa anakwenda kujiunga na timu hiyo Emiliano SalaPicha: Reuters/Action Images

Baba  yake  Sala  aliamka  jana  na  kufahamishwa  kwamba  ndege iliyosababisha  kifo  cha  mwanae  imepatikana. "Siamini. ni  ndoto mbaya  ninayoota," Horacio Sala  amesema  alipowasiliana  na kituo  cha  televisheni  cha  Cronica nyumbani  kwake  mjini Progreso.

 

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe / rtre / ape / dpae

Mhariri: Idd  Ssessanga