1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabomu ya mtawanyiko

Kalyango Siraj22 Februari 2008

Isreal yalaumiwa kwa kuyatumia

https://p.dw.com/p/DBiY

Mkutano kuhusu mabomu-mtawanyiko-yaani Cluster-Bombs uliokuwa unafanyaka nchini New Zealand umemalizika wakati serikali zaidi ya 122 zilizowakilishwa kuunga mkono hati ya mkataba inayopendekeza kupiga marufuku silaha hizo.

Mbali na yaliyofikiwa katika mkutano huo,mataifa muhimu duniani yanayotengezneza mabomu hayo kama vile China, Urusi, na Marekani, baado yanapinga marufuku ya moja kwa moja na hayakushiriki katika mkutano huo.

Mabomu haya ninayoita ya mtawanyiko-ambayo katika lugh geni yanaitwa Cluster Bombs,yanachukuliwa kuwa mabaya kutokana na muundo wake.

Ubaya wa mabomu haya ni kuwa bomu moja huwa na vijibomu vingine vidogovidogo ambavyo husambaa ama kutawanyika katika eneo kubwa.Vijibomu hivyo vidogo vinaweza kukaa kwa mda mrefu bila kulipuka na kuweza kulipuka baadae hata baada ya mgogoro uliosababishwa kutumiwa ukiwa ulikwisha malizika kwa miaka.wengi wa wahanga wa mabomu hayo ni raia wa kawaidia.

Mkutano wa Wellington- New Zealand-uliokuwa wa siku tano ni sehemu ya shughuli kadhaa zilizoanzishwa na kundi linaloweza kuitwa 'juhudi za Norway' zilizoanzishwa Febuari mwaka wa 2007 na kutarajiwa kufikia kilele chake kwa kupatikana kwa mkataba unaopiga marufuku matumizi ya silaha hizo katika mkutano wa Dublin utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu.

Mkutano wa New Zealand umeungwa mkono na mtandao wa ushirika dhidi ya silha za mabomu mtawanyiko ambao unaitwa kwa kifupi -CMC.Kundi hilo linaunganisha makundi ya kiraia 200 mkiwemo viongozi ambao walipata tuzo la Nobel kutokana na juhudi zao za kupinga mabomu yanayotegwa ardhini-maarufu kama landmines.

Ushirika huo umesema leo kuwa mataifa 82 yalitia saini kile kilichoitwa-Tamko la wellington- ambalo litasaidia majadiliano zaidi kulekea kuundwa kwa hati itakayopelekea kupiga marufuku mabomu hayo, kusaidia wahanga na pia kusafisha maeneo ambayo yanashukiwa kuwa na mabomu hayo.

Tamko la Wellington miongoni mwa mengine linasema kuwa,mabomu ya mtawanyiko husababisha maumivu yasio kubalika kwa raia wa kawaidia na matumizi yake,utengenezaji pamoja na usambazaji wake ni lazima yapigwe marufuku.

mapema wiki hii, ushirika huo,ulizilaumu serikali 9 ambazo zilitia sahihi hati hiyo kwa kujaribu kumaliza nguvu hati hiyo ili kuikubalia Marekani,kuendelea kuyatumia mabomu hayo.

Serikali hizo ni Japan,Australia,Finland, Ufaransa, Uholanzi,Ujeruamni, Uingereza, Denmark,na Uhispania.

Mratibu wa ushirika huo,Thomas Nash amesema kuwa jaribio la mataifa fulani kupunguza makali ya hati hiyo,halikufaulu,hata hivyo yatafikiriwa katika mkutano ujao uatakaofanyika Dublin.

Mwenyekiti mwenza wa ushirika huo,Steve Goose,mapema wiki hii,aliuambia mkutano wa waandshi habari kuwa mabomu hayo ndio silaha mbaya zaidi ya wakati huu,tangu mabomu ya kutegwa ardhini yapigwe marufuku mwaka wa 1997.

Takriban mataifa 76 yanashehena ya mabomu yao tayari kwa matumizi.

Nalo shirika linalotetea haki za binadamu la Human Rights watch liliilaumu Israel kwa kukiuka sheria ya binadamu za kimataifa kwa kutumia mabomu hayo kusini mwa Lebanon mwaka wa 2006.

Mabomu hayo yalianza kutumiwa katika vita vya pili vya dunia,wakati yakiitwa -mabomu vipepeo.tangu wakati huo mabomu hayo yametumiwa katika mataifa takriban 24,mkiwemo,Laos miaka ya 1960, Vietnam na Cambodia,Afghanistan,Afrika ,kosovo mwaka wa 1999 na Iraq pamoja na Lebanon.