1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko kisiwani Madagascar

Oumilkher Hamidou3 Februari 2009

Meya wa Antananarivo abadilshwa na serikali

https://p.dw.com/p/GmVK
Meya wa mji mkuu wa Madagascar Andry RajoelinaPicha: AP


Serikali ya Madagascar imempokonya wadhifa wake meya wa mji mkuu Antananarivo,Andry Rajoelina baada ya kusema ataunda serikali ya mpito mwishoni mwa wiki ijayo katika kisiwa hicho cha bahari ya hindi ikiwa rais atakataa kung'atuka.



Kwa muda wa wiki mbili sasa Andry Rajoelina,mwenye umri wa miaka 34 amekua akiongoza maelfu ya waandamanaji dhidi ya rais Marc Ravalomanana,anaemtaja kua "muimla."


Watu kadhaa wameuwawa kufuatia mapigano ya majiani,moto na hata visa vya kupora mali.


Vurugu hili jipya katika kisiwa hicho cha misuko suko cha Madagascar-kisiwa cha nne kwa ukubwa ulimwenguni,linatishia kuhatarisha shughuli za utalii na kufuja juhudi za nchi hiyo za kuwavutia wateja wa kigeni.


Serikali ya rais Marc Ravalomanana imemchagua Guy Rivo Randrianarisoa kushika nafasi ya Andry Rajoelina kama meya wa Antananarivo.


Rajoelina lakini alichaguliwa kwa kura za wananchi,hata hivyo mtaalam mmoja wa masuala ya sheria anasema kutimuliwa kwake madarakani ni sawa kisheria.


"Uamuzi wa serikali ni halali ikiwa itadhihirika kwamba meya huyo hatekelezi jukumu lake" amesema hayo Jean-Eric Rakotoarisoa ambae ni mtaalam wa masuala ya katiba.Hata hivyo anahisi itakua shida zaidi kuutekeleza kivitendo uamuzi huo kwasababu ya malalamiko ya wafuasi wake".Mwisho wa kumnukuu mtaalam huyo wa masuala ya kikatiba.


Andry Rajoelina aliuhutubia umati wa watu elfu mbili waliovalia nguvo za rangi ya machungwa hii leo akiahidi kutangaza serikali ya mpito  hadi ifikapo jumamosi ijayo ikiwa rais hatokubali kung'atuka kwa amani madarakani.


Marc Ravalomanana,tajiri mkubwa mwenye umri wa miaka 59 amesisitiza, bado anashuikilia hatamu za uongozi na kutoa mwito wa utulivu nchini.


Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon aliuambia mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa,"ameingiwa na hofu kupita kiasi"kutokana na hali namna ilivyo kisiwani Madagascar.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amezitaka pande zinazohusika ziufumbue mzozo wao kwa njia ya amani.


Umoja wa Afrika  umelaani kwa upande wake "aina yoyote ya njama kwa lengo la kumtoa madarakani rais Ravalomanana."


Rajoelina,kwa jina la utani TGV,linalolinganishwa na jina la treni ya mwendo wa kasi ya Ufaransa,ametuma maombi mbele ya baraza la katiba na bunge kutaka Ravalomanana apokonywe wadhifa wake.


Wakati huo huo polisi inasemekana imewakamata wapinzani sita jana walipokua wakijiandaa kuitisha maandamano katika mji wa kaskazini mashariki wa Toamasina.


"Wametaka kuitisha mkutano bila ya ruhusa"-amesema hayo mkuu wa polisi wa mji huo wa bandari.


Wadadisi wanakubaliana kwamba Rajoelina anajivunia uungaji mkono wa wananchi walio wengi waliovunjwa moyo na serikali,lakini pengine amezicheza vibaya karata zake kwa kujaribu kutaka kumpindua rais Ravalomanana.(Reuters)