1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko yadhibitiwa nchini Ufaransa

29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUPJ

Mamia ya maafisa wa polisi wameshika doria usiku wa kuamkia leo katika kitongoji cha mji wa Paris, Villiers-le-Bel, ambako vifo vya vijana wawili vilisababisha machafuko wiki hii.

Licha ya visa vya hapa na pale vya motokaa kuchomwa, kulikuwa na utulivu katika barabara na maeneo ya makaazi ya kitongoji cha Villiers-le- Bel, huku maafisa wa polisi wakishika doria na helikopta ya polisi ikizunguka anga ya kitongoji hicho.

Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, ameamuru uchunguzi huru ufanywe kuchunguza vifo vya vijana hao wawili viliyosababisha machafuko ya siku tatu. Rais Sarkozy pia ameapa kuwaadhibu watakaowafyatulia risasi polisi.

Maafisa 120 wa polisi walijeruhiwa wakati walipokuwa wakijaribu kuyazima mchafuko yaliyoanza Jumapili iliyopita.