1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID : Kumbukumbu ya miaka 3 ya uripuaji treni

11 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCK9

Uhispania imekuwa na kumbukumbu ya miaka mitatu ya kuripuliwa kwa treni mjini Madrid leo hii shambulio lililohusishwa na Waislamu wa itikadi kali lililopelekea kuuwawa kwa watu 191 na kujeruhi wengine karibu 2,000.

Mfalme Juan Carlos na Malkia Sofia pamoja na maafisa waandamizi wa serikali walihudhuria kuzinduliwa kwa mnara wa kumbukumbu nje ya kituo cha reli cha Atocha mojawapo ya vituo vine vilivyoshambuliwa.

Mabomu kadhaa yaliripuwa treni za abiria wakati wa harakati za asubuhi tarehe 11 mwezi wa Machi mwaka 2004 katika shambulio baya kabisa la kigaidi kuwahi kushuhudiwa barani Ulaya.

Watu 29 hivi sasa wanashtakiwa mjini Madrid kuhusiana na miripuko hiyo.