1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID.Mahakama kuu yawazuia wagombea kusimama katika uchaguzi wa serikali za mitaa

6 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4N

Mahakama kuu ya Uhispania imewazuia mamia ya wagombea kusimama katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika jimbo la kaskazini la Basque.

Wagombea hao wamedaiwa kuhusika na kundi lililopigwa marufuku la chama cha Batasuna.

Mahakama hiyo imepitisha uamuzi kwamba kundi la kisosholisti la Aberzale linaunga mkono juhudi za tawi la kundi la kisiasa linalopigania kujitenga kwa jimbo la Basque la ETA.

Kundi la ETA kwa zaidi ya miaka 30 limekuwa likiendesha kampeini za kupigania uhuru wa jimbo la Basque kaskazini mwa Uhispania na kusini magharibi mwa Ufaransa na kusababisha kuuwawa kwa zaidi ya watu 800.