1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maduro awahimiza wanajeshi kupambana na 'wasaliti'

Bruce Amani
3 Mei 2019

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amelitaka jeshi la nchi hiyo kumkabili yeyote anayepanga njama ya mapinduzi, baada ya uasi wa wanajeshi wanaomuunga mkono kiongozi wa upinzani Juan Guaido kuzimwa

https://p.dw.com/p/3HrS7
Venezuela Maduro ruft Armee zur Entwaffnung aller Putschisten auf
Picha: Reuters/Miraflores Palace

Akizungumza katika hafla iliyohudhuriwa na wanajeshi 4,500 kwa mujibu wa serikali, Maduro alisema kuwa hakuna anayeweza kuwa muoga, kwa sababu ni wakati wa kuilinda haki ya Amani ya nchi.

Waziri wa Ulinzi Vladmir Padrino alisema "walikusanyika kuonyesha utiifu wao kwa amiri jeshi mkuu ambaye ndiye rais pekee, Rais Nicolas Maduro.

Mnamo siku ya Jumanne, Guaido – ambaye anatambuliwa na zaidi ya nchi 50 kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo iliyogubikwa na mzozo – aliwaomba wanajeshi kumuondoa madarakani kiongozi huyo anayekabiliwa na shinikizo.

Kundi dogo liliitikia wito huo, lakini vuguvugu hilo likashindwa – uongozi wa kijeshi umetangaza kuiunga mkono serikali na Maduro anashikilia msimamo wake dhidi ya shinikizo la kimataifa.

Venezuela Caracas Leopolo Lopez vor der spanischen Botschaft
Kiongozi wa upinzani Lopez katika ubalozi wa UhispaniaPicha: Getty Images/AFP/J. Barreto

Wakati huo huo, mahakama ya juu ya Venezuela iliamuru kukamatwa tena kwa kiongozi wa upinzani mwenye ushawishi Leopoldo Lopez – ambaye alijitokeza kwa pamoja na Guaido Jumanne baada ya kutoroshoshwa kutoka kifungo cha nyumbani.

Serikali ilisema zaidi ya watu 150 walikamatwa Jumanne. Mpaka sasa, wanajeshi waasi 25 wamechukua hifadhi katika ubalozi wa Brazil. Akizungumza katika makazi ya balozi wa Uhispania, Lopez mwenye umri wa miaka 48 alisema uasi mdogo uliofanywa Jumanne mwishowe utaufikisha kikomo udikteta wa Maduro.

Uhispania imesema haitamkabidhi Lopez kwa serikali ya Venezuela, wala kumtaka aondoke ubalozini.

Mivutano nchini Venezuela imeongezeka tangu Guaido, anayeongoza bunge la nchi hiyo, alipoitumia katika kujitangaza kaimu rais mnamo Januari 23, akidai kuwa kuchaguliwa tena Maduro mwaka jana hakukuwa halali.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameionya serikali ya Venezuela kutotumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji, wakati Marekani na Urusi zikituhumiana kwa kuuchafua zaidi mgogoro huo kwa kutumia ugomvi wao wa enzi ya vita baridi.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Marekani Mike Pompeo na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov wanatarajiwa kuijadili Venezuela