1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu waandamana dhidi ya chama cha AfD

Sekione Kitojo
25 Septemba 2017

Mamia kwa maelfu ya watu waliingia mitaani katika miji kadhaa nchini Ujerumani jioni ya Jumapili(24.09.2017)wakipinga chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Alternative for Germany AfD,ambacho kitangia katika bunge.

https://p.dw.com/p/2kdHw
Deutschland Bundestagswahl- Proteste gegen AfD in Frankfurt
Picha: picture-alliance/dpa/A. Arnold

Chama  cha  AfD  kitangia  katika  bunge  la  shirikisho  Bundestag  kwa mara  ya  kwanza  katika  historia  yake  kufuatia  uchaguzi mkuu  wa  taifa uliofanyika  siku  ya  Jumapili.

Kiasi  ya  waandamanaji  1,000  walijikusanya   nje  ya  klabu  ya usiku  katika  eneo  la  Alexanderpatz  mjini  Berlin  ambako  chama cha  AfD  kilikuwa  kinafanya  sherehe  zake  za  kushangiria matokeo  ya  uchaguzi.

Waandamanaji  walipiga  makelele "  Ondokeni , Ondokeni ,  na  AfD , wabaguzi  duni !"

Deutschland Bundestagswahl- Proteste gegen AfD in Frankfurt
Mjini Frankfurt mamia kwa maelfu ya watu waliandamana kupinga chama cha AfDPicha: picture-alliance/dpa/A. Arnold

Mamia  kadhaa  ya  watu  pia  walijikusanya  kwa  ajili  ya maandamano  ya  ghafla  katika  mji  wa  mashariki  wa  Leipzig, Maandamano  mengine  yaliripotiwa  mjini  Kolon, Hamburg  na Frankfurt. Katika  maandamano  mjini  Kolon , ambapo  watu  karibu 400  walishiriki , yalikuwa  ni  sehemu  ya  kampeni  ya  nchi  nzima iliyopewa  jina  la  "siasa za  kizalendo sio  mbadala."

Mtandaoni  hashtag  moja  ilikuwa  ni  miongoni  mwa  mada   tano zilizokuwa  zikiwashughulisha  sana  watu  waliongia   katika mitandao  ya  jamii  katika  twitter  nchini  Ujeruimani  kwa  sehemu kubwa  ya  jioni.

Wale  ambao  hawakuunga  mkono  chama  cha AfD , ambacho kimepata  asilimia  13  ya  kura , walitumia  "hashtag 187percent" kusisitiza ukweli  kwamba  walipiga  kura  zao  kwa  vyama  vikuu.

Mmoja  wa  waandamanaji  Peter Palberg  amesema:

Deutschland Bundestagswahl | AfD Wahlparty | Petry
Mwenyekiti wa chama cha AfD Frauke Petry baada ya uchaguzi wa 2017 mjini BerlinPicha: picture alliance/dpa/B. Von Jutrczenka

"Hawa  ni  Wanazi tu. Ukiangalia  wanasiasa  wao  na  lugha wanayotumia. Inakumbusha  kwa  kiasi  kikubwa  enzi  zilizopita."

Kwa  wiki  kadhaa , kansela  Angela  Merkel  alilazimika  kukabiliana na  kuzomewa  na  miluzi kila  mahali  alikokwenda  katika  kampeni katika  jimbo  anakotoka  mashariki  mwa  Ujerumani. 

Wapiga kura wa  mashariki

Na  jana Jumapili, ilikuwa  ni  wapiga  kura  wa  mashariki, waliokasirishwa na  uamuzi  wake  wa  kuwaruhusu  wakimbizi mamia  kwa  maelfu kuingia  nchini  humo, ambapo  kulipelekea  kukipatia  chama  chake cha  kihafidhina  matokeo  mabaya  kabisa  tangu  mwaka  1949 na kusababisha  chama  cha  siasa  kali  za  mrengo  wa  kulia  kuingia bungeni.

Muandamanaji  mmoja Jonas Ockelmann  Berlin  alisema.

"Binafsi  nimeathirika  na  kuingia  kwa  chama  cha  AfD  katika bunge. Siasa  zao  zinaniathiri. Wanapinga  mashoga na wanawake. Hawataki  vitabu  vya kiada vinavyoonesha  wanawake wenye mahusiano  ya  kimapenzi."

Matokeo  hayo  yanaashiria  kwamba taasisi  zinazokusanya  maoni ya  wapiga  kura  huenda  walipuuzia  athari  za  mzozo  wa wakimbizi  katika  uchaguzi  huu  na  ushawishi  mkubwa  ambao ungepatikana  kutoka  upande  wa  mashariki mwa  Ujerumani, ambako  wapiga  kura  wanaendelea  kuwa  na  mwelekeo  tofauti kabisa  na  wenzao  wa  upande  wa  magharibi  miaka  28  baada ya  kuanguka  kwa  ukuta  wa  Berlin.

Deutschland Bundestagswahl | Protest gegen die AfD
Muandamanaji akionesha hasira zake dhidi ya chama cha AfD mjini BerlinPicha: Reuters/W. Rattay

Wakati  baraza  kuu  la  Wayahudi  nchini  Ujerumani  limesema ongezeko  la  uungwaji  mkono  kwa  chama  cha  AfD ni changamoto  kubwa  inayoikabili  Ujerumani  baada  ya  vita  vikuu vya  dunia , kiongozi  wa  chama  cha  siasa kali  za  mrengo  wa kulia  nchini  Ufaransa  Marine Le Pen amekipongeza  chama  cha AfD kwa  "matokeo  yao ya  kihistoria."

Nae  rais  wa  Ufaransa Emmanuel  Macron amempongeza  leo kansela  wa  Ujerumani Angela  Merkel  kwa  ushindi  wake, akiahidi kwamba  washirika  wawili  hao wa  Ulaya  wataendeleza  ushirikiano wao muhimu.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe / rtre

Mhariri: Zainab Aziz