1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu wakusanyika kumkumbuka Benazir Bhutto nchini Pakistan

Mohamed Dahman27 Desemba 2008

Takriban Wapakistani 200,000 leo wamekusanyika katika kaburi la waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto kwa kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kuuwawa kwake.

https://p.dw.com/p/GNko
Maelfu ya wafuasi wa marehemu Benazir Bhutto wakiwasili katika kaburi lake Jumamosi ya tarehe 27 Desemba huko Garhi Khuda Bakhsh karibu na Larkana nchini Pakistan kwa kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kuwawa kwake.Picha: AP

Baadhi yao wakiwa wametembea kwa miguu kwa mamia ya maili kuweza kufika hapo.

Bhutto aliuwawa kwa kupigwa risasi katika shambulio la kujitolea muhanga kwa kujiripuwa wakati akiondoka kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ya uchaguzi katika mji wa Rawalpindi nje kidogo ya mjii mkuu wa Islamabad hapo Desemba 27 mwaka 2007.

Mume wake Asif Ali Zardari alishika uongozi wa chama cha Bhutto baada ya kifo chake na alichaguliwa kuwa rais wa Pakistan hapo mwezi wa Septemba.

Waziri Mkuu Yousuf Raza Gilani amesema katika hotuba ya televisheni leo hii kwamba Bhutto aliwapa wananchi sauti na alikuwa ni matumaini ya wananchi wa Pakistan.

Umoja wa Mataifa umesema unataka kuchunguza kifo cha marehemu Bhutto.