1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maendeleo katika mazungumzo ya Kenya

15 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D7o2

NAIROBI:

Makundi yanayohasimiana kisiasa nchini Kenya,yamekubali kuwa na katiba mpya katika kipindi cha mwaka mmoja.Tangazo hilo limetolewa na mpatanishi wa serikali Mutula Kilonzo mjini Nairobi.Lakini makundi hayo mawili bado hayakuafikiana kuhusu suala muhimu yaani mfumo wa serikali mpya.

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan aliongoza majadiliano ya siku mbili kati ya wajumbe wa Rais Mwai Kibaki na wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.Annan hii leo katika mkutano wa waandishi wa habari,anatazamiwa kufafanua zaidi kuhusu maendeleo yaliyopatikana.

Wakati huo huo,Rais wa Marekani George W.Bush amesema,waziri wake wa Mambo ya Nje Condoleezza Rice atakwenda Nairobi siku ya Jumatatu kumsaidia Kofi Annan katika juhudi zake za upatanishi.Majadiliano ya upatanisho yanatazamiwa kuendelea siku ya Jumatatu mjini Nairobi.Machafuko yaliyozuka nchini Kenya kufuatia uchaguzi wa rais uliofanywa Desemba 27,yamesababisha zaidi ya vifo 1,000 nchini humo.