1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko Pakistan , watu zaidi ya 800 wafariki

Sekione Kitojo1 Agosti 2010

Zaidi ya watu 800 wamepoteza maisha yao katika mafuriko mabaya kuwahi kutokea kaskazini magharibi ya Pakistan

https://p.dw.com/p/OZEC
Wanakijiji nchini Pakistani wakihangaika kutaka kufika katika maeneo ya salama kutokana na mafuriko mabaya kabisa kuwahi kutokea nchini humo.Picha: ap

Zaidi ya watu 800 wamepoteza maisha yao katika mafuriko mabaya kabisa kutokea kaskazini-magharibi ya Pakistan katika kipindi cha miaka 80 iliyopita. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa takriban watu milioni moja wameathirika kwa mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa za msimu wa masika.

Waokozi kutoka Pakistan na nchi jirani ya Afghanistan wanawatafuta wakaazi waliokwama  katika vijiji vilivyozingirwa na maji. Ripoti zinasema watu 60 wameuawa katika eneo hilo. Madaraja yaliyobomoka na barabara zilizofurika zinachalewesha kazi za wasaidizi wanaotaka kupeleka misaada kwa wahanga waliokwama vijijini.

Umoja wa Mataifa umeahidi kupeleka misaada ya kiutu kwa wale walioathirika. Serikali ya Ujerumani imezidisha msaada wake kufikia Euro milioni 1. Wakati huo huo Umoja wa Ulaya utatoa msaada wa Euro milioni 30.Kwa mujibu wa idara ya utabiri  wa hali ya hewa, mvua huenda zikaendelea kunyesha kwa hadi siku kumi zingine.