1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

100810 Afrika Extremismus

Abdu Said Mtullya10 Agosti 2010

Ugaidi waenea barani Afrika vilevile asema mwandishi wetu Ute Schaeffer.

https://p.dw.com/p/Ohqd
Magaidi wajitandaza barani Afrika.Picha: AP

Ugaidi wa waislamu wenye itikadi kali katika bara la Afrika haupo nchini Somalia na katika nchi za kaskazini mwa bara hilo tu!

Ugaidi huo umekuwa unaenea katika bara hilo kutoka kaskazini hadi Afrika ya kati. Wanaoathirika ni wananchi wa kawaida.

Watu na hasa wafanyakazi katika mashirika ya misaada wanatekwa mara kwa mara. Katika eneo la Sahel wanaotekwa nyara aghalabu huwa watu kutoka nchi za magharibi.

Hivi karibuni mfaransa aliekuwa na umri wa miaka 78 alitekwa nyara na kuuawa. Mwishoni mwa mwezi uliopita mwili wake ulikutwa umetelekezwa.

Magaidi wamekuwa wanajitandaza barani Afrika kuanzia kusini mwa Algeria,Mauretania,Burkina Farso,Mali hadi nchini Niger.

Lakini kwa kwiango kikubwa ni watu wa eneo hilo lote wanaogeuka mateka . Kwani wengi wao wanategemea biashara ili kujiendeshea maisha yao, na katika miaka ya hivi karibuni walianza kutegemea shughuli za utalii Lakini sasa ugaidi unawapokonya watu hao msingi wa kuendeshea maisha yao.

Miongoni mwa watu hao ni watu wa kabila laTaureg.

Watu hao watambulika kwa malemba yao mazuri na makubwa ambayo yemekuwa kama nembo ya eneo lao la Sahara.

Lakini kwa sasa shughuli za utalii katika eneo lao zimenasa kutokana na ukosefu wa usalama, utekaji nyara na mauaji ya watalii kutoka nchi za magharibi.

Mano Aghali,wa kabila la Taureg ambae ni mbunge amesema maisha ya watu wake yameathirika kwa kiwango kikubwa, kaskazini mwa Niger na katika eneo la Agadez, kutokana na ugaidi. Aghali amesema magaidi wamewapokonya watu msingi wa maisha yao katika sehemu hizo.

Watu hao wanaishi kutokana na utalii. Wapo wale waliokuwa wanawaongoza watalii, madereva na wapishi na wachuuzi.Kinachoitwa "uasi 2007", na athari zake kilisababisha mshtuko mkubwa miongoni mwa watu hao.Kwa sababu watu hao wana mawezekano madogo sana ya kufanya kitu kingine.Wengi wao hawakuwa sehemu ya uasi huo na wala hawakushiriki katika mapambano.Lakini sasa wao pia hawana kazi.

Anachoita Mano Aghali uasi wa pili,ulianza mnamo mwaka wa 2007.Mashambulio ya kivamizi yaliyofanywa katika vituo vya polisi na kambi za wanajeshi, mapambano baina ya waasi na wanajeshi.Hali ya wasiwasi ilienea kaskazini mwa Niger.Lakini uasi huo ambao seriali inauita upinzani ulikuwa tofauti na wapo awali ambapo watu kabila la Taureg walipigania maisha bora katika eneo lao na kushiriki katika maamuzi ya kila siku ya eneo lao.Wimbi jipya la umwagikaji damu kuanzia mwaka wa 2007 halihusiani na malengo ya kisiasa yaliyopiganiwa na wataureg.

Waliochochea mgogoro hasa ni watu wanaonufaika na biashara ya mihadarati na silaha.Watu hao wameziteka nyara harakati za wataureg .Na wakati wote wamekuwa wanajificha nyuma ya wimbo ule ule wa wataureg." Tupambane kwa ajili ya wataureg, tupiganie maendeleo ya jimbo la Agadez"

Mbunge wa wataureg Mano Aghali alieanzisha asasi ambayo si ya kiserikali anadhamiria kuwafungulia watu wake fursa za elimu na maendeleo.

Mwandishi/Schaeffer Ute/

Tafsiri/Mtullya Abdu/

Mhariri/.Josephat Charo