1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: Juncker akutana na Trump

Sekione Kitojo
26 Julai 2018

Wahariri wa magazeti  ya hapa  Ujerumani wamejishughulisha  na  mkutano  kati ya  Donald Trump na  rais wa halmashauri ya Umoja  wa  Ulaya Jean-Claude Juncker , hukumu iliyotolewa kuhusiana  na utafiti wa  vinasaba.

https://p.dw.com/p/326si
USA Washington Jean-Claude Juncker, Präsident EU-Kommission & Donald Trump
Picha: Reuters/J. Roberts

Mhariri  wa  gazeti la  Mittelbayerische Zeitung la  mjini  Regensburg anazungumzia  kuhusu  mkutano  kati  ya  rais  wa  halmashauri  ya Umoja  wa Ulaya  Jean-Claude Juncker  na  rais  wa  Marekani Donald Trump.  Mhariri  anaandika:

"Trump kwa  kweli  hana  mwelekeo  wa  kufanya  mambo  kwa  haki, badala  yake  anataka kutamalaki. Kwa  hiyo  anajaribu, kuugawa Umoja  wa  Ulaya. Badala  ya  kufanya  mikataba  na  mataifa makubwa  ambayo yana  uwezo  sawa  na  Marekani , anajaribu kutafuta  mikataba  na  mataifa  madogo  madogo, ambayo  anaweza kuyapeleka  vile  anavyotaka. Na  anatumia  njia  ya  kutoa  misaada na  kuondoa  ushuru."

Gazeti  la  Flensburger Tageblatt  likizungumzia  mada  hiyo  ya mkutano  kati  ya  Trump  na  Juncker  linaandika  kwamba  Donald Trump  anatoa  sifa  kwa  mkutano  wa  kilele  wa  G7  na  washiriki wake, lakini  anakataa  kutia  saini  tamko  la  pamoja  la mkutano huo. Mhariri  anaandika:

"Ndio  sababu  Kim Jong Un amekuwa  mwerevu , ambaye anawapenda  watu  wake, kwa  kuwa  mtu  anapata  kitisho ,akikumbuka  kile  kilichomtokea  Gaddafi , aliyeuwawa  baada  ya nchi  yake  kushambuliwa  kwa  makombora  ya  NATO. Kwa  kifupi , Trump  kama  muwamba  ngoma anapenda  kuvutia  kwake. Na matokeo  yake  bila  shaka  ni Marekani  kwanza. Lakini  je  hayo ndio  maajabu  pekee  ya  mtu  huyu  ama  kuna mbinu  nyingine zaidi?"

Kuhusiana  na  mada  juu  ya  uamuzi  wa  mahakama  juu  ya  utafiti wa  vinasaba, mhariri  wa  gazeti  la  Landeszeitung  la  mjini Lueneburg  anaandika:

"Mashine  ya  inayosaga  unga  kwa upande  wa  mahakama  inasaga taratibu, lakini  inaleta  unga  laini kabisa. Kwa  muda  wa  miaka mitano watafiti  walikuwa  wahangaika  na  matokeo  ya utafiti  wao wa  vinasaba  kuhusiana  na mimea. Mahakama  ya  Ulaya hatimaye imetoa  hukumu , kwamba  ubadilishaji  wa  vinasaba  vya asili na  kuingizwa  vinasaba  vya vigeni  katika  mmea  ni  mbinu  tu za  utafiti  na  sio utaratibu  wa kilimo kinachoweza  kutumika moja kwa  moja."

Mhariri  wa  gazeti  la Koelner Stadt-Anzeiger, kuhusiana  na  uamuzi wa  mahakama  ya  juu  ya  utafiti  wa  vinasaba, anaandika:

"Watumiaji  wanapaswa  kufahamishwa  vizuri  zaidi juu  ya mbinu za vinasaba, ili  kwa  karibu  waweze  kutoa  maamuzi  yao  kuhusiana na kilimo  hicho. Matumizi  ya  mazao  yanatokana  na  utaalamu  huo yaweze  kuwa  bora  zaidi. Hatari  inaweza  kuepukwa. Na  kwa  hiyo hali  ya  matumizi  ya  mazao  yaliyobadilishwa  vinasaba  haitakuwa na  matatizo  tena  hata  kwa  watu  wanaopendelea  mbegu  za asili."

Mhariri  wa  gazeti  la  Emder Zeitung  anazungumzia  kuhusu  joto na  mioto  inayowaka  misituni. Mhariri  anandika:

"Suala  moja  liko  wazi  hapa, mhariri  anaandika  kwamba  hali  hiyo ya  hewa  itaendelea  kuwa mbaya  zaidi.  Hii  ni  moja  kati  ya matokeo  ya  dunia  yetuinayotumia  mbinu  nyingi  za  kiufundi. Imetuwi  vigumu  sana  kuweza  kuchukua  hatua  kutokana  na  hali kama  hizo  ambazo  si  za  kawaida. Kila  siku  hususan  katika  siku za  kazi, kila  kitu  kinakwenda  kama  kilivyo. Watu  wanakuwa kama  mashine  katika  hatua  za  uzalishaji, bila  kujali , iwapo  nje kuna  lundo  la  barafu  ama   kuna  uhaba  wa  maji. Utaratibu  huu unatuonesha  kwamba  binadamu  ni  sehemu  tu  viumbe  na  licha ya  kuwa  na uwezo  wa  ufundi  lakini  hatuwezi  kudhibiti uasili."

Sudi:

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / inlandspresse

Mhariri:Yusuf Saumu