1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: Kura ya Brexit kuamua hatimaya Uingereza na EU

Sekione Kitojo
15 Januari 2019

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani  wamejishughulisha leo na suala la kura itakayopigwa katika bunge la Uingereza kuhusu Brexit, na  pia mzozo wa kidiplomasia kati ya Marekani na Uturuki.

https://p.dw.com/p/3BZRz
England: Symbolbild Brexit
Picha: Reuters/H. Nicholls

Tukianza  na  gazeti  la  Mannheimer Morgen, kuhusu  Brexit  mhariri anaandika:

"Wakati  tukielekea  katika  suluhisho linalohitajika , tatizo  halipo  kwa Umoja  wa  Ulaya , badala  yake ni  utekelezaji  wa kisiasa wa waziri mkuu  wa  Uingereza Theresa  May  . Masuala  ya   uzalendo , kujifaharisha si  mambo  yanayoweza kutosheleza  na  kuwafanya watu  kuamini. Na  kwa  uwazi  watu  wangeweza  kusema  hatua  hii ya  Brexit  inaleta  uharibifu  mkubwa kwa  nchi  yetu."

Mhariri  wa  gazeti  la Oberhessische Presse  anaandika   kuhusu Brexit kuwa  Umoja  wa  Ulaya  pia  unahitaji  mabadiliko: Mhariri anaendelea:

"Wiki chache  kabla  ya  uchaguzi  wa  bunge  la  Ulaya  kuna  hatari ya  mataifa  wanachama  kutumbukia  katika mparaganyiko, kwa kuwa  uchaguzi  huo  unataka kuutupa mkono  Umoja  huo. Mamilioni ya  watu  katika  nchi  nyingine  za  Umoja  wa  Ulaya  watafahamu hivi  sasa, kwamba  EU ni  jinamizi  la  umangimeza, ambapo wananchi  wake wanawekewa  tu maelekezo  yasiyostahili , na kwamba  yale  matamko  ya  mara  kwa  mara  ya  wanasiasa  ya kwamba  kila  kitu  kiko  sawa , sio  kweli.

Si  kila  kitu  kinakwenda  vizuri  katika  Umoja  wa  Ulaya, na  hilo linaelezewa  pia  na  wabunge  wa  Umoja  huo, hali  ambayo inaifanya  Uingereza  kutotaka  pia  kubakia  katika  Umoja  huo. Umoja  wa  Ulaya  mhariri  anaandika, unahitaji  mabadiliko na hili  ni suala  gumu."

Kuhusu  suala  la  mzozo  wa  kidiplomasia  kati  ya  Uturuki  na Marekani, mhariri  wa  gazeti  la  Freie Presse anaandika:

"Hadhi  ya  Marekani  inavurugika  kunapotokea  mara  suala  hili mara  lile  katika  mashariki  ya  kati.  Marekani  ambayo   hadi  sasa ni  nchi  pekee  yenye  nguvu  inachukua  hatua  nusu  nusu  katika kutekeleza  jukumu  lake  katika  kila  uamuzi  kutoka  pale  rais atakapoandika  katika  ukurasa  wa  Twitter  hadi mara  nyingine. Baadhi  katika  eneo  hilo  la  mashariki  ya  kati  wanamatumaini , kwamba  huenda  hakutakuwa  na  kitu  chochochte  kitakachotokea hadi  wakati  mwingine  uchaguzi  wa  Marekani  utakapomalizika."

Nalo gazeti  la Nueremberger  Nachrichten linaandika  kuhusu maandishi  wa  rais  Trump  katika  ukurasa  wa  Twitter. Mhariri anaandika:

"Donald  Trump kwa  mara  nyingine  tena  amefanikiwa, kwa maandishi  katika  ukurasa wa  Twitter  kuiweka Uturuki  ambayo  ni mwanachama  wa  NATO  katika  mapambano dhidi  yake, nafasi yake kama  mpatanishi  katika  mashariki  ya  kati ameishusha  na wakati  huo  huo  nafasi  ya  Urusi  nchini  Syria  kuiimarisha. Trump anataka  kuyaondoa  majeshi  yake , lakini  wakati  huo  huo aweze kupambana  na  wanamgambo  wanaojiita  Dola  la  Kiislamu  pamoja na  ushawishi  wa  Iran.  Hali  hii  inaharibu  sifa  ya  marekani  katika mashariki  ya  kati."

Kwa muhtasari  hayo  ndio  yaliyoandikwa  na  wahariri  wa magazeti ya Ujerumani  hii  leo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse

Mahriri: Yusuf, Saumu