1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: Mkutano wa NATO, Trump aishambulia Ujerumani

Sekione Kitojo
12 Julai 2018

Maoni ya wahariri wa magazeti ya  Ujerumani yanazungumzia kuhusu mkutano wa kilele  wa  jumuiya  ya  NATO, pamoja  na hukumu  aliyopewa mwanamke ambaye alituhumiwa  kuwa mmoja wa  magaidi  hapa Ujerumani Beate Zschaepe.

https://p.dw.com/p/31KZt
Belgien Brüssel Pressekonferenz Donald Trump
Rais Donald Trump wa MarekaniPicha: picture-alliance/AP Photo/G. Vanden Wijngaert

Mhariri  wa  gazeti  la  Rheinpfalz la mjini  Ludwigshafen anazungumzia  kuhusu mkutano wa  NATO  na  ukosoaji wa  rais  wa Marekani Donald Trump kwa Ujerumani.

Mhariri  anaaandika  kwamba Muuzaji  ambaye anagombana  na wanunuzi  wake  anaharibu  kazi  yake. Bila  shaka  rais  wa Marekani Donald Trump  ndivyo  anavyofanya. Kwa anataka Marekani  iuze  gesi  nyingi  zaidi asilia kwa  bara  la  Ulaya, anaishambulia  Ujerumani  kutokana  na  kuagiza  gesi nyingi na  hali hiyo  anaiita  kuwa "mfungwa  wa  Urusi. Kwa  hiyo sio tu mzozo wa kibiashara  wa  Trump, lakini  pia  matamshi yake  ya  kijinga yanaharibu  muonekano wa  Marekani. Kuishutumu  Ujerumani kwamba  inaifanya Urusi  kuwa tajiri na  pia  kwamba  Ujerumani itakuwa inaitegemea  zaidi Urusi  ni  jambo  lisilo  na  msingi. Kwa miongo  kadhaa  mataifa  ya Ulaya  yamekuwa  yakitegemea  gesi kutoka  katika  eneo  la  Siberia. Kama mshiriam wa  kibiashara Urusi  wakati  huo  ilikuwa yenye  kuaminika kuliko ilivyokuwa Marekani. Madai ya Trump sio ya  kweli  kama  zilivyo  hesabu  zake. Ujerumani  haipati  mahitaji  yake  ya nishati  kwa  asilimia  70 kutoka Urusi, lakini  chini  ya  asilimia  40  tu.

Nae mhariri  wa  gazeti  la Hannoversche Allgemeine Zeitung akizungumzia  mkutano  wa  kilele  wa  NATO  anasema, sentensi muhimu kuhusiana  na  siasa  za  Marekani  chini  ya  Trump aliisema  Merkel  zaidi  ya  mwaka  mmoja  uliopita  katika  hema la bia  mjini  Munich katika  eneo  la tamasha la  bia kule Trudering. Wakati  huo  Merkel  alisema, muda ambapo tumezowea  kubweteka, umepita. Watu wa Ulaya  tunapaswa  kuelekeza mustakabali  wetu wenyewe. Matamshi  haya  ndio  kwanza  tunayabaini. Mataifa  ya Ulaya, hususan  Ufaransa na  Ujerumani, yanapaswa  kujitafakari , kwamba anaweza  kuondoa  mwanvuli unaotulinda  na silaha za kinyuklia. Na  baada  ya  hapo? Huenda  kikosi  cha  kupambana  na silaha  za  kinyuklia  cha  Ufaransa  kilichopo Ulaya  ya  kati kikalazimika  kuingilia  kati. Kwa  hali  halisi  ya  hivi  sasa  huenda isiwe  hivyo.  Huenda  matumizi  ya  asilimia  2 ya pato jumla  la  taifa haitakuwa kiwango  cha  mwisho. Tunaweza  kufikia  haraka  lengo hilo  la  asilimia  2, kuliko tunavyopenda, iwapo  Trump atavuruga uchumi  wa  dunia  kupitia  vita  vya  kibiashara. Asilimia  2 inaweza kufikiwa  bila  ya  kuchukua  hatua  zaidi, kwa  kuwa  inawezekana kutokana  na  kunywea  kwa uchumi.

Kuhusu  hukumu  dhidi ya  Beate Zschaepe mwanamke  anayedaiwa kuhusika  na  kundi  la  kigaidi, gazeti  la  Weser-Kurier la  mjini Bremen,  linaandika  kwamba, wakili wa Zschaepe  tayari alishasema, kwamba  atakata  rufaa  dhidi  ya  uamuzi  wa mahakama  hiyo. Wakili  anadai  kwamba  mwanamke  huyo mwenye umri  wa  miaka  43 hakuwahi  kabisa  kuhusika  katika  tukio  la shambulizi, kutambua  kuwa hajawahi  kuhusika kabisa na watu waliofanya  mashambulizi.  Hali  hiyo inaweza  kuleta msisimko mkubwa, kwasababu  kundi  hilo  la  washambuliaji  linafahamika  kwa kiwango  kikubwa  walikuwa wakifanya  shughuli  zao  kwa  karibu sana.

Naye mhariri  wa  gazeti la  Allgemeine Zeitung  la  mjini  Mainz akizungumzia  kuhusu  hukumu dhidi  ya  idara ya  NSU linasema historia  ya  NSU ni  historia  ya kushindwa  vibaya  katika jamhuri ya Ujerumani. Kwa miaka  mingi  kumekuwa na wasi wasi  wa kundi  la mauaji na lilionekana  kuwa  halihusiki na  mauaji  hayo. Na  kundi lililokuwa  likiwasaidia  lilitathminiwa  kuwa  na  kiasi  ya  watu 100 hadi 200.  Wengi  wao  bado  hawajulikani  ama  hawajatiwa  hatiani.

Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse / deutschland

Mhariri: Mohammed Khelef