1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini:Kampeni zapamba moto uchaguzi wa Ujerumani

Sekione Kitojo
12 Septemba 2017

Magazeti ya leo(12.09.2017)yameandika zaidi kuhusu kampeni za uchaguzi hapa  Ujerumani, uharibifu uliotokea baada ya kimbunga Irma na mjadala kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, na pia kuhusu ligi ya mabingwa barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/2jn2T
Lübeck ARD-Wahlarena mit Bundeskanzlerin Merkel
Picha: picture-alliance/dpa/D. Reinhardt

Tukianza  na  gazeti  la  Badische Neueste Nachrichten la  mjini Karlsruhe, linazungumzia  kuhusu kampeni  za  uchaguzi  nchini Ujerumani kwa  ajili  ya  uchaguzi utakaofanyika  hapo Septemba  24. Mhariri  anaandika:

Katika mapambano  ya  vyama kuwania  kushika  nafasi  ya  tatu  hili ni  suala, linalohusu  idadi ya viti  na  heshima, nani atakuwa  juu  ya vyama  vingine  vidogo. Kwa  wakati  huu  hakuna  jibu ,  lakini  swali linaendelea  kubaki , Ujerumani  itakuwaje  baada  ya  uchaguzi, serikali ijayo  itakuwaje itaundwa  na  vyama  gani na  mwelekeo gani  itachukua. Swali  hili hakuna  anayeweza  kulijibu , baina  ya Merkel  na martin Schulz na ni  kwamba kila  kitu  kiko  wazi , na mwishowe baadhi  ya  vyama  vidogo  ndio vitaamua  ni  aina  gani ya  serikali  ya  mseto itaundwa.

Baadhi  ya  watu  wanazungumzia  dhidi  ya  muungano  uliopo  sasa wa  chama  cha  CDU  na SPD, yaani  muungano  unaojulikana kama  wa  rangi  nyeusi  na  nyekundu. Mhariri  wa  gazeti  la  Rhein-Neckar-Zeitung la mjini  Heidelberg anazungumzia  kuhusu muungano huo  mkuu  pamoja na  chama  cha  siasa  kali  za  mrengo  wa  kulia cha  AfD.

Huenda  basi chama  cha  AfD kingekuwa  chama  kikuu  cha upinzani , kingepata  haki  ya kuzungumza  bungeni  kama  sehemu ya  serikali kivuli. Bila  shaka  wanainchi  wa  Ujerumani wangelazimika  kukubaliana  na  hali  hiyo. Lakini  ni  kutokana  na kulazimika  tu. Martin Schulz  kutoka  chama  cha  SPD awe kiongozi wa  upinzani. Huo  hautakuwa uchaguzi  mbaya.

Mada  nyingine  ni  kuhusu maafa  yaliyosababisha  na  kimbunga Irma. Mhariri  wa  gazeti la Südwest-Presse  la  mjini  Ulm anaandika:

USA, Florida | Hurrikan Irma
Kimbunga Irma kikishambulia maeneo nchini MarekaniPicha: Reuters/C. Barria

Kiwango  cha  juu  cha  joto  cha  maji  katika  maeneo  ya  tropiki kinasababisha  mabadiliko  ya  hali  ya  tabia  nchi. Uharibifu mkubwa  uliofanywa  na  kimbunga Harvey  na  Irma  nchini Marekani  ni  matokeo  ya  kudharau  mabadiliko  hayo. Marekani inapaswa  kujichunguza  binafsi. Wamarekani  wanapaswa kumfahamisha  rais  wao  kwa  utulivu  kabisa, kwamba  chungu kikichemka maji hutoka kupitia  mvuke.

Gazeti  la  Aachener Nachrichten  linazungumzia  kuhusu  michuano ya  Champions League inayoanza  rasmi  leo  kwa  awamu  ya makundi.

Michuano  hiyo  inaanza  rasmi  leo, lakini  mhariri  anaiangalia  zaidi klabu  ya  Paris St. Germain  ambayo imetumia  fedha  nyingi  msimu huu  kujiimarisha.

Mhariri  anasema  rais  wa  shirikisho  la  kandanda  barani  Ulaya Aleksander Ceferin  hana tatizo na  kuifungia  klabu  kama  Paris St. Germain kucheza  katika  Champions League , lakini  kuizuwia  klabu hiyo  ya Ufaransa  inayopata fedha  kutoka kwa masheikh  wa ghuba kufanya  mchezo wanaoucheza na klabu  hiyo na kuzuwia mchezo wa  mpira  kuharibika hilo halitatokea.  Klabu  hiyo inayomilikiwa  na masheikh kutoka  Qatar watatoa hatimaye msaada kidogo kwa shirikisho  hilo , halafu kila  kitu kitakwenda kama kilivyo.

 

Mwandishi : Sekione  Kitojo /  Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman