1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini:Mahakama ya Ulaya imeamua sahihi dhidi ya Hungary

Sekione Kitojo
7 Septemba 2017

Wahriri wa magazeti ya Ujerumani leo(07.09.2017)wamezungumzia uamuzi wa mahakama ya Ulaya kugawana wahamiaji barani Ulaya, ripoti juu ya hali ya Ujerumani kuhusu uchumi kati ya iliyokuwa Ujerumani mashariki na magharibi.

https://p.dw.com/p/2jV61
Europäischer Gerichtshof in Luxemburg
Jengo la mahakama ya sheria ya Umoja wa Ulaya mjini LuxemburgPicha: Reuters/F. Lenoir

Pia wahariri kadhalika  wameandika  kuhusu  madhila yanayowakuta Waislamu  Warohingya nchini  Myanmar

Tukianza  na  gazeti  la  Rhein Zeitung  la  mjini  Koblenz kuhusu mada  ya  wakimbizi na  wahamiaji mhariri  anaandika

Mahakama  ya  Ulaya  imefikia  uamuzi  sahihi.  Mashitaka yaliyotolewa  na  Hangary  katika  mahakama  hiyo  ya  Luxemburg yametolewa  hukumu  ya  haki kabisa. Kwasababu  haiwezekani kwamba nchi  mwanachama  linataka  kubadilisha  uamuzi , ambao inaupendelea tu, na Umoja  wa  Ulaya  hauwezi  kufanyakazi  kwa njia  hiyo na  hautafanya  hivyo  katika  siku  zijazo. Umoja  huu umejengeka  katika  msingi  wa  kuwapo  tayari  kuwa na maridhiano, na  ni  hilo  pekee  litaleta  maendeleo.

Nalo  gazeti  la Frankfurter  Allgemeine Zeitung  kuhusu  mada  hiyo linaandika:

Umoja  wa  Ulaya  ulipitisha  azimio  kuyasaidia  mataifa  yaliyoko mstari  wa  mbele  katika  mzozo  huu  wa  wakimbizi, Italia  na Ugiriki  kuwagawa  wakimbizi  wapatao 120,000  kwenda  katika mataifa  mengine  ya  Umoja  huo  katika  muda  wa  miaka  miwili.

Ndipo  Hangury  na Slovakia , kwa  kuungwa  mkono  na  Poland , zilipeleka  mashauri  katika  mahakama  ya  sheria  ya  Ulaya kupinga  azimio  hilo.  Ni  haki  kabisa  kwa mujibu  wa  sheria , kwa mashitaka  kama  hayo  kushindwa.

Gazeti  la  Badische Neueste Nachrichten  la  mjini  Karlsruhe linazungumzia  kuhusu  ripoti  ya usawa  wa  kiuchumi  nchini Ujerumani  baina  ya  ujerumani  mashariki  na  magharibi. Mhariri anaandika.

Ujenzi  wa usawa  wa  hali  ya  maisha  ni  jukumu  muhimu  sana  la majimbo  yote  nchini  Ujerumani.  Zaidi  ni  kuimarisha  uwezo  wa majimbo yale yenye uchumi dhaifu ili kuzuwia  kuporomoka  zaidi. Bila hivyo itakuja  hali  ya mtengano  baina  ya  majimbo  yenye  hali bora  ya  kijamii  na  yale  ambayo  hali  yake  ni  mbaya. Hii italeta hali  mbaya  katika  amani  ya  ndani.

Mwishowe  ni mada  kuhusu  madhila  yanayowapata  Waislamu  wa Rohingya  nchini  Myanmar. Mhariri  wa  gateti  la  Rheinpfalz  la mjini  Ludwigshafen  anaandika.

Kile  kinachotokea  katika  eneo  la  kaskazini magharibi  mwa Myanmar ,kwa  kweli  ni  vigumu kukitathmini. Wachunguzi wasioelemea  upande  wowote  wanazuiwa  kuingia  katika  eneo hilo la  machafuko.  Lakini  kila  mzozo  huo  wa  Warohingya unavyoendelea , ndivyo  hali  inavyozidi  kuwa ya  wasi  wasi  zaidi na  Waislamu  wa  Rohingya  wanaendelea  kukimbilia  Bangladesh na  katika  mataifa  mengine ya  jirani. Jinsi Myanmar inavyowafanyia Warohingya  sio  tena  mzozo  ambao ni  wa Myanmar  pekee.

Alikuwa sekione  Kitojo  aliyetukusainyia  maoni  ya  wahariri  wa magazeti  ya  Ujerumani  leo  hii.

Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse

Mhariri: Yusuf , Saumu