1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini:Theresa May aahirisha mjadala wa Brexit Uingereza

Sekione Kitojo
11 Desemba 2018

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamezungumzia kuhusu vuta nikuvute kuhusu mjadala wa Brexit nchini Uingereza, mkataba wa uhamiaji wa Umoja wa Mataifa, na mgomo wa tahadhari wa madereva wa treni nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/39qxV
Niederlande Theresa May, Premierministerin Großbritannien & Mark Rutte
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May(kushoto) akipokelewa na waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte (kulia)Picha: picture-alliance/AP Photo/P. Dejong

Tukianza  na  gazeti  la  Badische Neueste  Nachrichten  la  mjini Karlsruhe , linazungumzia  kuhusu mtafaruku  unaojitokeza  katika mchakato  wa  Brexit  nchini  Uingereza. Mhariri  anaandika:

"Kuahirishwa ghafla  kwa  mjadala  mkali  kuhusiana  na  makubaliano ya  kujitoa  kutoka  Umoja  wa  Ulaya  kumeepusha  Theresa  May kuagukia  pua  kisiasa na  kudhalilika. Lakini  fadhaa  hiyo ya  Brexit anairefusha  tu. Waziri  mkuu  huyo  wa  Uingereza  ana  matumaini kwamba, kundi  kubwa  linaloongezeka  la  wakosoaji  wake  litakata tamaa. Wakati  huo  huo  anataka  kuongeza  mbinyo  kwa  Umoja wa  Ulaya, huku  muda  mfupi  uliobakia  hadi Uingereza kujitoa kutoka  Umoja  wa  Ulaya   Machi  29  kukisogea. Lengo  la waziri mkuu  ni  kwamba,   mataifa  ya  Umoja  wa  Ulaya  yataipa Uingereza wakati  ikijotoa vitu vitamu  na  kuzuwia  kabisa  Brexit ambayo  ina  masharti."

Waziri  mkuu  wa  Uingereza  ameweza kwa  ukakamavu  na bila kuyumbishwa  kuendelea  na  mradi  wake  mkuu  katika  kipindi  cha karibu  miaka  miwili  na  nusu  ya utawala  wake,  anaandika  hivyo mhariri  wa  gazeti  la  Schwäbische Zeitung  la  mjini  Ravensburg. Mhariri  anaendelea:

"Amefanya  hivyo  kutokana  na  matakwa  ya  wananchi  ya  kujitoa kutoka  Umoja  wa Ulaya pamoja  na  makubaliano  na  Umoja  huo mjini  Brussels. Makubaliano  hayo  ya  kujitoa  pamoja  na  ufafanuzi wa  kisiasa  ambao  kwa  washirika  wengi  wa  Ulaya  bara  kwa kiasi  kikubwa  wanataka  kupata maridhiano, wengine  wakitaka kufika  mbali  zaidi  katika  muafaka. Mjini  London  lakini  kuna hakuna  kabisa  hali  ya muafaka na  makubaliano.  Wale  wateteaji wakubwa  wa  Brexit ambao  ni  Boris Johnson  na  Jacob Rees-Mogg wanataka  mwishoni  mwa  mwezi  Machi  kujitoa  bila makubaliano  yoyote. Hali  hii  inaweza  kuleta  matatizo  makubwa ya  kiuchumi  kwa  mataifa  ya  Ulaya  pamoja  na  Ireland, na  hata kwa  Waingereza  wenyewe."

Katika  suala  la  mkataba  wa  Umoja  wa  Mataifa  wa  uhamiaji , mhariri  wa  gazeti  la  Ludwigsburger Kreiszeitung  anaandika kwamba  hofu  kuhusu  uhamiaji  ni  kuhusu utekelezaji. Mhariri anaandika:

"Kumekuwa  na  hali  ya  kupinga maelezo  ya utekelezaji  wa kutokulazimika kisheria, ambapo hatimaye  unazungumzia  tu  kuhusu biashara  ya  bianadamu, kama  ilivyo  utaratibu  hapa  Ujerumani kwa  muda  mrefu. Mataifa  mengi  yako  katika  mbinyo  kutokana na  mkataba  huu  kuachana  na  siasa  zao  za  kizalendo. Nchini Ubelgiji hali  hiyo ilisababisha serikali  kuporomoka. Ni hali  ya uharibifu kimataifa. Iwapo  tutaanza, kulazimika  kuomba  radhi, kwamba  tuko  katika  hali  mbaya  ya  dharura na  kuonesha  sura ya  urafiki, mhariri  anaandika  kwamba, hapo  hiyo  si  nchi  yangu tena. Hayo  ameyasema Angela  Merkel  mwishoni  mwa  mwaka 2015. Kuonesha  urafiki kidogo, pia  ni  ubinadamu. Na  hapo  kuna mpaka. Na  pia  kuonesha ushirikiano  wa  pamoja   kimataifa."

Mhariri  wa  gazeti  la  Frankfurter Allgemeine Zeitung anazungumzia kuhusu  mgomo  wa  madereva  wa  treni  nchini  Ujerumani. Mhariri anaandika:

"Matatizo  mengi  ya  treni  ni  ya  ndani. Lakini  katika  hali  ya  sasa ya  mgomo  wanaowajibika  ni chama  cha  wafanyakazi  wa  huduma za  treni. Wanapaswa  kujiuliza , iwapo mgomo  wao wa tahadhari wa  nchi  nzima  ulikuwa  ni  sahihi. Hawakutilia  maanani  kuhusu wengi  wa  wasafiri kufika  makazini  na  wakawasababishia matatizo  makubwa.  Mfumo  mzima  wa  usafiri , iwe  kwa  reli, barabara, maji  ama  angani  ulikuwa  ulifikia  ukomo  wake. Hata hivyo  ni  mara  chache  kwa  mfumo  huo  kufanyakazi  bila matatizo."

 

Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse

Mhariri: Josephat Charo