1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magufuli arejesha matumaini Tanzania

9 Desemba 2015

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amekonga nyoyo za Watanazania kwa mikakati yake ya kuokoa fedha za umma, ikiwemo kufuta sherehe za uhuru na badala yake kuitumia siku hiyo kufanya usafi.

https://p.dw.com/p/1HJik
Unabhängigkeitstag Tanganyika Independence Day 9.12.
Picha: Said Michael

Rais John Magufuli aliushangaza umma wa Watanzania pale alipotangaza uamuzi wake wa kufuta sherehe za maadhimisho ya siku y auhuru mwaka huu. Hakungekuwepo na sherehe za matumizi makubwa zinazoambatana na hotuba, muziki na chakula. Badala yake Magufuli alitoa agizo kwa raia kuitumia siku ya Desemba 9 kwa kufanya usafi mitaani na majumbani kwao.

Katika mwezi wa kwanza wa uongozi wake, Magufuli ameendelea kusimama kwa jina laek la utani la "Tingatinga". Akidhamiria kupunguza matumizi yasiyo ya laazima ndani ya serikali, rais huyo wa awamu ya tano, ametangaza kupunguza idadi ya wajumbe watakaoshiriki mkutano wa mwaka wa jumuiya ya Madola nchini Malta kutoka 50 hadi wanne tu.

Na ametangaza huko mbeleni, ni rais, makamu wake na waziri mkuu pekee yao watakaokuwa na haki ya kusafiria madaraja ya juu katika ndege. Maafisa wengine wote wa serikali watasafiria madaraja ya kawaida. Magufuli pia alikata bajeti ya dhifa ya kitaifa ambayo kwa kawaida huambatana na uzinduzi wa bunge. Pesa hizo zilizoookolewa zimetumika kununulia vitanda katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli alipokula kiapo kuiongoza Tanzania.
Rais Magufuli alipokula kiapo kuiongoza Tanzania.Picha: Reuters/E. Herman

Nini atakachokifanya Magufuli

Hatua hizo alizozichukuwa rais Magufuli zinaonekana kumgeuza nyota kwenye mitandao ya kijamii. Watu wamebuni hata tungo za maneno kama vile "Magulify" likimaanisha "kuitangaza hatua haraka au kwa gharama nafuu; kuwanyima uwezo watumishi wa umma, kufurahia maisha kwa gharama ya walipakodi, kuwaogofya watumishi wazembe na wala rushwa katika jamii."

Kwa hashtaga ya #WhatWouldMagufuliDo, maelfu wametumia mtandao wa kijamii wa Twitter kulezea ni namma gani walitaka kutumia pesa juu ya kitu lakini wakabidili mawazo baada ya kumkumbuka Magufuli. "Nilitaka kutoka kwa ajili ya chakula cha mchana, lakini baadae nikajiuliza#WhatWould MagufuliDo? Nimeishia kula sandwich." Mtumiaji huyo aliweka picha mbili za mkate na barafu.

Raia kutoka nchi jirani ya Kenya hasa wanatumia mitandao ya kijamii kueleza namna wangependa kuwa na rais kama Magufuli. "Wakenya wanaamini ni hatua nzuri kwa Tanzania kuwa mfano mzuri. Pengine rais wetu atafuata mfano huo na kupunguza matumizi ya serikali ili Wakenya wame na maisha bora," alisema mwandishi wa habari wa Kenya Fred Ng'etich katika mahojiano na DW.

Onyo kwa watumishi wazembe

Magufuli ameapa kupambana na watumishi wazembe serikalini na kutumia fedha za serikali kwa ufanisi zaidi. Amekososa waziwazi vitendo vya rushwa na ubadhirifu ndani ya chama chake tawala CCM, ambacho kimakaa madarakani tangu mwaka 1977. "Natoa ilani kwa watumishi wazembe serikalini kukaa chonjo: Wamevumiliwa kwa muda mrefu, huu ndiyo mwisho wao," alionya katika hotuba yake ya kwanza kwa bunge.

RAis Magufuli akilihutubia bunge.
RAis Magufuli akilihutubia bunge.Picha: DW/H. Bihoga

Hata upinzani unakiri kuwa huu umekuwa mwanzo mzuri kwa rais. lakini kuna hofu kuwa Magufuli anafanya kazi na kuchukuwa maamuzi kivyake bila kuzingatia sheria zilizopo. "Sisi kama bunge, tuna wajibu wa kuunga mkono juhudi zake za kuongeza uwajibikaji nchini, lakini tunapaswa kuhakikisha kuwa haya yote yanfanyika kwa kuzingatia sheria na kanuni," alisema Zitto Kabwe, moja wa wanasiasa wa upinzani bungeni.

Magufuli ametumia muda mrefu kuliko rais yeyote wa Tanzania kuunda baraza la mawaziri. Chaguo lake la mbunge asiyekuwa maarufu sana Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu, huenda ikawa ishara kuwa kutakuwa na sura mpya zaidi kwenye baraza lake kuchukuwa nafasi za vigogo wa CCM. Wakati wa kampeni zab urais, chama cha CCM kilichagua kaulimbiu ya "Hapa Kazi tu", ikimaanisha awamu hiyo ya tano itakuwa ni ya vitendo zaidi. Miaka mitano ijayo itaonyesha iwapo Magufuli anaweza kudumu na kaulimbiu hiyo.

Mwandishi: Elizabeth Shoo/DW

Tafisri: Iddi Ssessanga

Mhariri: Mohammed Khelef