1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri 19 tu, wengine hawana manaibu

Mohammed Khelef10 Desemba 2015

Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametangaza baraza lake la mawaziri likiwa na mawaziri 19 na wizara nyengine zikiwa hazina hata manaibu waziri ili kupunguza gharama.

https://p.dw.com/p/1HLBG
Rais John Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais John Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Picha: Reuters

Akitangaza baraza hilo leo (Disemba 10) Ikulu ya Magogoni, jijini Dar es Salaam, Magufuli alisema zilikuwa zimetengwa shilingi bilioni 2 ili mawaziri watakapoteuliwa waende semina elekezi, lakini baraza lake halitakuwa na semina hiyo badala yake fedha hizo zitaelekezwa kwenye sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure.

Mwandishi: Mohammed Khelef
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman