1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama DRC yamhukumu Kamerhe kwenda jela miaka 20

Sekione Kitojo
20 Juni 2020

Mahakama kuu  ya  jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, imempata  na  hatia mkuu wa ofisi ya rais Vilal Kamerhe kwa ubadhirifu wa  dola milioni 48 fedha  za  umma  na  kumhukumu kwenda  jela  miaka 20, jaji kiongozi amesema.

https://p.dw.com/p/3e5dS
Kongo Oppositionsführer Vital Kamerhe
Vital KamerhePicha: Imago/Belga/T. Roge

 Vital Kamerhe ni mwanasiasa  mwandamizi zaidi kubabiliana na kesi  ya rushwa nchini Congo, ambako kuna kiwango cha  ulaji rushwa. Jaji Pierrot Bankenge Mvita  amesema  kuwa kutokana na  kila  mtu aliyesikilizwa , mahakama  imeonelea  kuwa  kweli ubadhirifu wa  fedha  za  umma  zinazofikia kiasi  cha dola za Marekani  48,831,148.

DR Kongo Vital Kamerhe Politiker
Mnadhimu mkuu wa ofisi ya rais ya rais wa DRC ,Vital KamerhePicha: Imago Images/Belga/P. Deconinck

Kamerhe  anakana  kuiba  fedha  hizo zilizotengwa kwa  ajili ya  nyumba  za serikali  chini  ya  mpango  wa  rais Felix Tshisekedi  wa  siku 100 za  ujenzi. Kamerhe alimuunga  mkono rais Felix Tshisekedi katika  kampeni  ya  uchaguzi  ya  mwaka 2018 kwa matarajio ya  Tshisekedi kumuunga  mkono Kamerhe  katika  uchaguzi  wa mwaka 2023.

Mwanasiasa  huyo  mkongwe mwenye ushawishi  mkubwa  katika  kuunda  serikali alikuwapo katika  mahakama hiyo  ya  wazi iliyoketi  kwa  muda  wa  masaa  matatu akivalia  sare ya jela  yenye rangi za buluu  na  njano  na  pia  alivalia  barakoa kumlinda  dhidi  ya  virusi  vya corona. Kukamatwa  kwake  hapo Aprili 8 kulileta wimbi  la  mshituko  katika  muungano unaounda  serikali  nchini  humo pamoja  na  taifa  lote kwa  jumla.

Bildkombo Felix Tshisekedi und Vital Kamerhe
Picha inayowaonesha rais Felix Tshisekedi (kushoto) na Vital Kamerhe (kulia)

Wiki iliyopita  waziri  wa  sheria alifichua kuwa  jaji wa  zamani, ambaye alisemekana  hapo mwanzo kuwa  amefariki kwa  ugonjwa  wa  moyo mwezi  uliopita, alikuwa  ameuwawa kinyama.