1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya ICC yatupilia mbali ombi la serikali ya Kenya

Aboubakary Jumaa Liongo30 Agosti 2011

Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu ya The Hague leo imetupilia mbali ombi la serikali ya Kenya kutaka kusikilizwa nchini humo kwa watuhumiwa sita wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

https://p.dw.com/p/12Q4y
Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga wakitia saiani makubalianao ya kuunda serikali ya pamoja babada ya ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007Picha: picture-alliance/ dpa

Akisoma uamuzi huo hii leo Jaji Hans-Peter Kaul amesema uamuzi wa kusikilizwa kwa kesi hiyo kwenye mahakama ya The Hague uliyotolewa tarehe 30 Mei mwaka huu ni sahihi baada ya kutoridhishwa na vigezo vya upande wa walalamikaji ambao ni serikali ya Kenya.

Amesema serikali imeshindwa kutihibitisha kuwa inaendelea na uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo, kama ilivyoahidi wakati wa kuwasilisha ombi lake hilo.Pia amesema kuwa hakuna ushahidi uliyothibitisha kuwa mashahidi katika kesi hiyo walihojiwa na serikali ya Kenya.

Jaji Kaul akizidi kuelezea sababu za kutupilia mbali ombi hilo la serikali ya Kenya amekubaliana na hoja ya mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo Luis Moreno Ocampo ya kwamba uwezo wa serikali hiyo kushughulikia kesi za ndani haukidhi mahitaji ya kusikilizwa kwa kesi za uhalifu wa kiwango hicho kama kinavyotakiwa na mahakama hiyo ya ICC na hivyo kutaka kusikilzwa kwa kesi hiyo nchini Kenya ni kuchelewesha pasipo na lazima mchakato mzima wa kesi hiyo.

Serikali ya Kenya iliwasilisha ombi la kutaka kusikilizwa nchini humo kwa kesi hiyo ikidai kuwa katiba mpya pamoja na mabadiliko yaliyofanywa katika mfumo wa sheria yanakidhi matakwa ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Uamuzi huo umetolea hii leo muda mfupi tu baada ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali ya Kenya Amos Wako na Waziri wa sheria Mutula Kilonzo kukanusha madai ya mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Luis Moreno Ocampo ya kwamba serikali ya Kenya inaihujumu mahakama hiyo ya ICC na kuwa inawalinda watuhumiwa hao sita kwa sababu za kisiasa.

Kesi hiyo sasa aitasikilizwa tarehe mosi mwezi ujayo yaani keshokutwa kama ilivyopangwa hapo awali.Watuhumiwa hao ni pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha Uhuru Kenyata, aliyekuwa Waziri wa Elimu ya Juu na mbunge wa Eldoret William Ruto, Francis Muthaura, Hnery Kosgey na Mkuu wa zamani wa Polisi Mohammed Hussein.Rutto na Uhuru Kenyata wameshaonesha nia ya kutaka kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujayo ambapo Rutto na Kosgeyi Waziri wa zamani wa viwanda waliondoka jijini Nairobi leo alfajiri kuelekea The Hague.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/Reuters/ICC web

Mhariri:Mohamed Abdul-Rahman