1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Kenya yazuia Ujenzi wa mtambo wa makaa ya mawe

Amina Mjahid
26 Juni 2019

Korti ya Mazingira nchini Kenya imezuia kwa muda ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe, ambao ulitarajiwa kujengwa katika kisiwa cha Lamu.

https://p.dw.com/p/3L8g5
Kenia Nairobi Demonstration gegen Kohlekraftwerk
Picha: Reuters/Baz Ratner

Mradi huo wenye gharama ya dola bilioni mbili umepingwa vikali na wanaharakati wa ulinzi wa mazingira, na wenyeji wa kisiwa hicho. 

Jaji Mohammed Balala ameubatilisha uamuzi wa awali ulioridhia kibali cha ujenzi kwa mwekezaji, Amu Power.

Balala amewataka wawekezaji kufanya tathmini mpya ya athari za kimazingira, ambazo mtambo huo unaweza kusababisha katika kisiwa cha Lamu kilicho katika Bahari ya Hindi, ambacho kimeorodheshwa na shirika la UNESCO miongoni mwa Turathi za dunia. 

Kampuni ya Amu Power inazo siku thelathini za kukata rifaa. Mahakama pia imesema umma wa Kenya haukushauriwa ipasavyo kuhusu mradi huo wa umeme unaozalishwa kwa makaa ya mawe, ambao ungekuwa wa kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki.