1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama yaridhia Kabila kuendelea madarakani

Sekione Kitojo
18 Oktoba 2016

Mjini Kinshasa leo (18.10.2016)vyama vinavyoshiriki katika serikali vimetia saini makubaliano yanayotoa ruhusa kuchelewesha uchaguzi uliotarajiwa kufanyika katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo mwezi ujao.

https://p.dw.com/p/2ROQZ
Kongo Präsident Joseph Kabila
Picha: picture-alliance/AP Photo/J. Bompengo

Vyama vinavyounda muungano tawala katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na vyama vingine vidogo vimekubaliana kuchelewesha uchaguzi wa mwezi ujao hadi Aprili mwaka 2018. Vyama  hivyo  vimetia saini makubaliano hayo mjini Kinshasa leo(18.10.2016). Makubaliano hayo yanatoa nafasi kwa Rais Joseph Kabila kusalia madarakani hadi uchaguzi mpya utakapofanyika.

Mkataba  huo ulipitishwa  baada  ya  mazungumzo yaliyodumu kwa  takriban siku  40, chini ya usimamizi wa mjumbe wa Umoja wa Afrika Edem Kodjo, licha ya kususiwa na vyama muhimu vya upinzani, kikiwemo UDPS cha kinara wa upinzani Etienne Tshisekedi.  Makubaliano hayo hayafafanui iwapo  rais Kabila  anaweza  kuwania  muhula mwingine  baada  ya  mwaka  huo.

Bildkombo Etienne Tshisekedi Joseph Kabila Demokratische Republik Kongo
Kinara wa upinzani Etienne Tshisekedi (kushoto) na kulia ni rais Joseph KabilaPicha: picture alliance/dpa/DW-Fotomontage

Mahakama ya katiba katika  nchi hiyo vile vile imekubali ombi  lililowasilishwa  na  tume ya  taifa  ya uchaguzi la kuahirishwa uchaguzi wa rais na bunge uliotarajiwa kufanyika  mwaka   huu. Hata hivyo mahakama  hiyo imeitaka tume  hiyo  ya  uchaguzi kutangaza kalenda mpya ya uchaguzi.

Vyama  ambavyo  havikushiriki  katika  majadiliano  hayo vinadai  kwamba  Rais Kabila  kubaki  madarakani kupindukia  muda  wake  anaoruhusiwa  na  katiba  ni kukiuka  katiba  ya  nchi  hiyo.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / DW Kinshasa correspondent.

Mhariri: Daniel Gakuba.