1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahujaji wa kipalestina wazichoma moto kambi

31 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CiNl

Zaidi ya mahujai 1,000 wa kipalestina wamezichoma moto kambi za muda huko Sinai mapema leo zilizojengwa na serikali ya Misri ili kuwahifadhi mpaka mgogoro juu ya vipi watakavyorejea katika Ukanda wa Gaza utakapotanzuliwa.

Mahujaji hao wa kipalestina waliwasili kwa basi katika kambi hizo 11 katika mji wa El Arish katika pwani ya bahari ya Mediterania jana Jumapili lakini wakakataa kukaa katika kambi hizo wakipinga juhudi za Misri kuwataka warejee makwao katika Ukanda wa Gaza kupitia kivuko cha mpakani cha Aouja kinachosimamiwa na Israel.

Mahujai hao wamepiga kelele za kumshutumu rais Hosni Mubarak wa Misri na serikali yake kwa kukataa kuwaruhusu warudi kwao kupita Rafah, ambako Israel haina wanajeshi wake.

Wanawake kadhaa wamezimia kutokana na moshi mweusi uliotanda anga ya eneo hilo la Sinai na kupelekwa hospitalini kwa matibabu.