1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majadiliano ya Amani - Mashariki ya Kati

14 Septemba 2010

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas, hii leo wanakutana kwa majadiliano ya amani katika Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/PBfB
US Secretary of State Hillary Rodham Clinton, left, meets with Palestinian President Mahmoud Abbas, in Sharm El-Sheikh, Egypt Tuesday, Sept. 14, 2010. Clinton said the "time is ripe" for Mideast peace, but that without face-to-face talks Israel can't expect lasting security and the Palestinians can't create an independent state.(AP Photo/Alex Brandon, Pool)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton(kushoto) akikutana na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas, Sharm-el-Sheikh, Misri.Picha: AP

Mkutano huo wa siku mbili unaanza katika mji wa Sharm el-Sheikh nchini Misri na utaendelea mjini Jerusalem chini ya uongozi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton.

"Sisi ni washirika wenu. Na nyie je? Hayo ni maandishi mapya yaliyopo katika mabanga yaliyoenezwa katika barabara za Tel Aviv kwa lugha ya Kiyahudi. Karibu na mabanga hayo, kuna picha za wanasiasa wa Kipalestina wanaoshiriki katika majadiliano ya amani chini ya uongozi wa Rais Mahmoud Abbas.

Hata kwenye mtandao wa intaneti, Wapalestina wanajaribu kuuvutia umma wa Israel kuhusu duru hii mpya ya majadiliano ya amani. Kwa mfano, kwenye tovuti ya wanaharakati wa Kiisraeli na Kipalestina,"Geneva Initiative" mpatanishi mkuu wa Wapalestina Saeb Erekat anajaribu kuwavutia Waisraeli:

"Ninawasalimuni huko Israel. Najua kuwa tumewavunja moyo. Najua kuwa miaka 19 iliyopita hatukuweza kupata amani.Najua kuwa wengi wa Waisraeli wanataka suluhisho la kuwepo madola mawili, kama Wapalestina wengi wanavyotaka pia. Najua kuwa amani inaweza kupatikana na itapatikana. Tutafanikiwa kupata amani. Mimi ni mshirika wenu.Je,nyinyi ni washirika wangu?"

Kundi la Geneva Initiative linajumuisha wanasiasa wa Kiisraeli na Kipalestina ambao miaka saba iliyopita waliwasilisha rasmi mpango ambao hadi hii leo unatumika kama kiegezo cha makubaliano ya amani ya Mashariki ya Kati yatakayopatikana.

Hata hivyo ,siku chache tu baada ya kufunguliwa duru mpya ya majadiliano ya ana kwa ana mjini Washington, kumezuka hatari ya majadiliano hayo kutofanikiwa. Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu anashikilia kuwa ule muda wa kusitisha sehemu ya ujenzi wa makaazi ya Walowezi katika Ukingo wa Magharibi unamalizika mwisho wa mwezi huu wa Septemba kama ilivyopangwa. Yeye angependelea kuruhusu upya ujenzi wa makaazi, angalao katika mitaa mikubwa ya wahamiaji wa Kiyahudi bila ya vizuizi.

Wakati wa mchakato wa amani wa Annapolis katika mwaka 2007 na 2008, Marekani kama mpatanishi iliruhusu hilo. Lakini safari hii, Wapalestina hawapo tayari kufanya majadiliano hayo tete wakati makaazi ya walowezi yakiendelea kuongezeka katika maeneo yao. Wapalestina wameonya kuwa watatoka kwenye ukumbi wa majadiliano ya Sharm-el-Sheikh ikiwa Netanyahu hatorefusha muda wa kuzuia ujenzi wa makaazi hayo.

Kwa maoni ya Yitzhak Herzog, waziri wa masuala ya jamii wa chama cha Leba cha Netanyahu, ni muhimu kuhakikisha kuwa majadiliano hayo yataendelea. Anasema,ujenzi wa makaazi hayo usitishwe kwa miezi miwili au mitatu mingine, lakini baadae uruhusiwe kuendelea kama kawaida.

U.S. Secretary of State Hillary Rodham Clinton, left shakes hands with Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu during their meeting at the Red Sea resort of Sharm el-Sheikh, Egypt Tuesday Sept. 14, 2010. Clinton said the "time is ripe" for Mideast peace, but that without face-to-face talks Israel can't expect lasting security and the Palestinians can't create an independent state. (AP Photo/Nasser Nasser)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Hillary Clinton(kushoto) na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu walipokutana Sharm-el-Sheikh, Misri.Picha: AP

Lakini Netanyahu anahisi kuwa anawajibika zaidi kutimiza matakwa ya walowezi wa Kiyahudi na serikali yake inayoelemea mrengo wa kulia kuliko yale ya Wapalestina. Amesema:

"Tunasema kuwa suluhisho ni kuwepo kwa mataifa mawili na jamii mbili - yaani taifa la Wayahudi na taifa la Wapalestina."

Lakini hata katika suala hilo hakuna msimamo mmoja. Wapalestina hawapo tayari kuitambua Israel kama taifa la Wayahudi kwani asilimia 20 ya wakaazi wa Israel ni Waarabu.

Mwandsishi: Engelbrecht,Sebastian/ZR/Martin,Prema

Mpitiaji:Mohammed Abdul-Rahman