1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majeshi ya Israel yauwa wawili.

13 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cou7

Gaza.

Shambulio la anga la majeshi ya Israel limeuwa wapiganaji wawili wa chama cha Hamas na kumjeruhi mwingine vibaya kusini mwa ukanda wa Gaza. Hamas kimethibitisha kuwa kombora moja lilishambulia eneo la kijeshi katika mji wa Khan Yunus na kwamba wanajeshi hao wawili waliouwawa wanatoka katika kundi la kijeshi la chama hicho.