1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majeshi ya Ujerumani yaondoka Kunduz

20 Oktoba 2013

Vikosi vya jeshi la Ujerumani vimeondolewa kutoka jimbo la Afghanistan la Kunduz muongo mmoja baada ya majeshi hayo kuwasili katika jimbo hilo.

https://p.dw.com/p/1A2jH
HANDOUT - Der Konvoi der Bundeswehr aus Kundus mit 441 Soldaten und mehreren Schützenpanzern vom Typ Marder fährt am 19.10.2013 früh morgens kurz vor Masar-i-Sharif. Zehn Jahre nach Beginn des Bundeswehr-Einsatzes in Kundus haben die letzten deutschen Soldaten die nordafghanische Unruheprovinz verlassen. Der Konvoi sei am Freitagabend in Kundus aufgebrochen und habe das Camp Marmal in Masar-i-Scharif ohne Zwischenfälle am Samstagmorgen erreicht. Foto: Bundeswehr/PAO RC N (ACHTUNG: Nur zur redaktionellen Verwendung im Zusammenhang mit der Berichterstattung und der vollständigen Nennung der Quelle) +++(c) dpa - Bildfunk+++ pixel
Wanajeshi wa Ujerumani wameondoka KunduzPicha: picture alliance/empics

Hatua hiyo inawakilisha hatua muhimu kuelekea kuondolewa kwa majeshi ya NATO nchini humo.

Miaka kumi baada ya Ujerumani kuanza kuweka majeshi yake katika jimbo lenye matatizo la kunduz ,jeshi la Ujerumani Bundeswehr limetangaza kuwa limefikisha mwisho ujumbe wake jana siku ya Jumamosi(19.10.2013).

"Tumekamisha kwa mafanikio operesheni ya "kujiondoa", amesema luteni kanali Heiko Diehl baada ya kuwasili katika kituo cha jeshi la Ujerumani nchini Afghanistan katika mji wa Mazar-i-Sharif.

HANDOUT - Der Konvoi der Bundeswehr aus Kundus mit 441 Soldaten und mehreren Schützenpanzern vom Typ Marder fährt am 19.10.2013 früh morgens kurz vor Masar-i-Sharif. Zehn Jahre nach Beginn des Bundeswehr-Einsatzes in Kundus haben die letzten deutschen Soldaten die nordafghanische Unruheprovinz verlassen. Der Konvoi sei am Freitagabend in Kundus aufgebrochen und habe das Camp Marmal in Masar-i-Scharif ohne Zwischenfälle am Samstagmorgen erreicht. Foto: Bundeswehr/PAO RC N (ACHTUNG: Nur zur redaktionellen Verwendung im Zusammenhang mit der Berichterstattung und der vollständigen Nennung der Quelle) +++(c) dpa - Bildfunk+++ pixel
Mlolongo wa magari ya jeshi la Ujerumani ukiondoka KunduzPicha: picture alliance/empics

Kukamilika kwa hatua ya Ujerumani kuviondoa vikosi vyake pia kumesifiwa na kamanda wa eneo hilo wa jeshi la kimataifa linaloongozwa na NATO linalotoa msaada wa usalama kaskazini mwa Afghanistan, meja jenerali Jörg Vollmer.

Wajivunia mafanikio

"Tunajivunia kile wanajeshi wetu walichofanikisha katika jimbo la Kunduz hadi katika dakika ya mwisho walipokuwa hapo," amesema Vollmer.

Jeshi la Ujerumani Bundeswehr lilikabidhi rasmi kambi yao kwa jeshi la usalama la Afghanistan katika sherehe iliyofanyika hapo Oktoba 6.

Hata hivyo , operesheni za usafirishaji zilichukua muda zaidi, ambapo majeshi yaliwasili hatimaye katika mji wa Mazar-i-Sharif asubuhi ya Jumamosi.

Mlolongo wa magari 119 , ikiwa ni pamoja na magari chapa Marder ya kivita , na wanajeshi 441 wamesafiri kilometa 300 kwa siku mbili.

Kuwekwa kwa jeshi la Ujerumani katika jimbo la Kunduz kunawakilisha mara ya kwanza kwa majeshi hayo kuhusika katika mapambano tangu vita vikuu vya pili vya dunia.

GettyImages 104650358 FEYZABAD, AFGHANISTAN - OCTOBER 02: German Bundeswehr soldiers patrols a street as Afghan police men walk past on October 2, 2010 in Feyzabad, Afghanistan. Germany has more than 4,500 military forces in Afghanistan as part of the US-led International Security Assistance Force. (Photo by Miguel Villagran/Getty Images)
Wanajeshi wa Ujerumani wakiwa na polisi wa AfghanistanPicha: Miguel Villagran/Getty Images

Sherehe hapo kabla mwezi huu zilihudhuriwa na waziri wa mambo ya kigeni Guido Westerwelle na waziri wa ulinzi Thomas de Maiziere, ambaye alisema katika hotuba kuwa Kunduz ilikuwa "sehemu muhimu sio tu kwa jeshi la Ujerumani Bundeswehr, lakini pia jina Kunduz linabaki kuwa alama ya mashambulizi ya anga yaliyoamrishwa katika eneo hilo ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 100 na kuwajeruhi wengine 11 Septemba mwaka 2009, wengi wao wakiwa ni raia.

Msaada bado waendelea

Kwa hatua hiyo , kituo cha Mazar-i-Sharif kinakuwa cha mwisho kwa Ujerumani nchini Afghanistan. Hata hivyo operesheni katika jimbo la Kunduz bado zinaendelea , kutokana na kuwapo wanajeshi 300 wa dharura ambao watawekwa katika eneo hilo ili kusaidia majeshi ya Afghanistan.

Operesheni ya Kunduz imedumu takriban kwa miaka kumi kamili, ambapo vikosi vya kwanza vya ujerumani viliwasili katika eneo hilo Oktoba 25, 2003. Uwekaji wa jeshi hilo katika eneo hilo la jimbo jirani la Baghlan umethibitisha kuwa miongoni mwa maeneo ya hatari sana kwa majeshi ya Ujerumani, ambapo wanajeshi wengi waliuwawa kuliko kokote kwingineko.

German Defence Minister Thomas de Maiziere (C) and Foreign Minister Guido Westerwelle (L) are welcomed by German Bundeswehr armed forces General Joerg Vollmer (R) upon their arrival in Camp Mamal in the northern city of Mazar-e-Sharif October 6, 2013. REUTERS/Fabrizio Bensch (AFGHANISTAN - Tags: MILITARY POLITICS)
Waziri wa ulinzi Thomas de Maizière (kulia)na Guido Westerwelle(kushoto) wakiwa katika kambi ya MamalPicha: Reuters

Zaidi ya wanajeshi 3,800 wanabakia nchini Afghanistan , ambapo zaidi ya wafanyakazi 5,350 wa jeshi hilo wakiwa katika eneo hilo wakati operesheni hizo zikiwa katika kwango chake cha juu. Zaidi ya wanajeshi 1,400 wa Ujerumani walikuwa Kunduz kwa wakati mmoja.

Baada ya marekani na Uingereza, Ujerumani ndio ilikuwa inachangia wanajeshi wengi zaidi katika jeshi hilo la kimataifa linalosaidia kuweka usalama nchini humo.

Majeshi ya kimataifa yanatarajiwa kufikisha mwisho operesheni za mapambano mwishoni mwa mwaka 2014, na kusafisha njia baadaye kwa ujumbe wa msaada wa mafunzo kulisaidia jeshi la Afghanistan.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rc/mkg(AFP,DPA) DW-English web

Mhariri:Caro Robi