1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majimbo 5 ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yakabiliwa na utapiamlo

15 Desemba 2010

Tatizo hilo limesababishwa na sera mbaya za kilimo

https://p.dw.com/p/QZnT
Mtoto wa Kiafrika anayekabiliwa na utapiamloPicha: AP

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limeelezea kwamba majimbo matano kati ya kumi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yamekumbwa na utapia mlo. Sababu ni kwamba kuna siasa mbovu ya kilimo na chakula kwenye maeneo hayo. Taarifa hiyo imetolewa kufuatia ripoti ya mwaka ya shirika la WFP kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na inaelezea kwamba hali ya ukosefu wa chakula katika maeneo mengine nchini humo inatia wasi wasi mkubwa.