1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makaa ya Msumbiji

Mohamed Dahman18 Januari 2013

Tokea kugundulikana kwa akiba kubwa ya makaa ya mawe, Tete, jimbo la kati la Msumbiji, limekuwa likivutia watu wengi kwa imani ya kutengeneza pesa kwa haraka. Lakini je, makaa hayo ya mawe yanaweza kutosheleza watu wote?

https://p.dw.com/p/16vxw
WER: vom brasilianischen Bergbauunternehmen Vale betriebene Mine in Moatize WO: vom brasilianischen Bergbauunternehmen Vale betriebene Mine in Moatize, Tete-Provinz, Mosambik WANN: Juli 2012 AUTOR: Marta Barroso
Picha: DW
WER: vom brasilianischen Bergbauunternehmen Vale betriebene Mine in Moatize WO: vom brasilianischen Bergbauunternehmen Vale betriebene Mine in Moatize, Tete-Provinz, Mosambik WANN: Juli 2012 AUTOR: Marta Barroso
Mgodi wa Moatize inaminika kuwa ndio mkubwa kabisa dunianiPicha: DW

Tete kwa muda mrefu imekuwa sio kitu cha kuzungumziwa na takriban hakuna mtu anayekwenda mwenyewe kwa hiari katika jimbo hilo lisilokuwa na harakati katikati ya Msumbiji ambalo linajulikana kwa  kuwa na joto la kiwango cha juu. Lakini leo jimbo hilo linajulikana kuwa ni jimbo lenye fursa kubwa kutokana na kugundulika kwa akiba kubwa ya makaa ya mawe miaka michache iliopita ambayo yumkini ikawa ndio akiba kubwa kabisa ya makaa ya mawe duniani. Kampuni nyingi za migodi za kimataifa zimekimbilia katika jimbo hilo hapo mwaka 2007 kwa nia ya kutengeneza pesa kwa haraka.

Ukiangalia kwa mbali huwezi kuona mengi ziada ya bonde jeusi! Kwenye bonde hilo kuna milima myeusi iliokoza na ukiikaribia unakuja kugunduwa kuwa hiyo ni milima mikubwa ya makaa ya mawe ilioko kwenye migodi ya Moatize katika jimbo la Tete nchini Msumbiji. Migodi hiyo inaendeshwa na kampuni ya migodi ya Brazil inayoitwa Vale na wafanyakazi wa migodi hufanya kazi usiku na mchana. Kila gari kubwa la mizigo linalopita hapo husafarisha hadi tani 400 za makaa ya mawe.

Maendeleo ya haraka

Kampuni ya Vale imewekeza takriban dola bilioni mbili katika awamu ya kwanza ya uchimbaji wa makaa hayo ya mawe. Katika kipindi cha miaka 35 ijayo kampuni hiyo inatarajiwa kuchimba tani bilioni mbili za makaa ya mawe kutoka ardhini. Mbali na hayo mkuu wa kampuni hiyo nchini Msumbiji Paulo Horta anasema kampuni yake hiyo inachangia maendeleo ya jimbo hilo. Anaamini kwamba miji ya Tete na Moatize inafaidika sana sio tu kutokana na kampuni ya Vale bali pia na makampuni mengine. Anasema hadi sasa wamewafunza vijana mia sita kutoka jimbo hilo ili waweze kufanya kazi kwenye migodi yao. Ameongeza kusema kwamba kutokana na watu hao kuhitaji chakula na mahala pa kuishi, jambo hilo limepelekea kuwepo kwa nguvu za kiuchumi zinazoleta taathira kwa jamii ya wenyeji wa Tete na Moatize.

Kwa kweli hali ya furaha imetanda katika mji wa Tete. Ardhi ambayo hapo zamani ilikuwa imetelekezwa leo kumesimama majengo mapya. Takriban hoteli zote huwa zimejaa na zile ambazo hazina wageni zinakuwa zinasubiri wafanyakazi wa kampuni kubwa.Kuna mikahawa mipya na katika kila pembe kunauzwa nguo na chakula.Hususan kuna benki nyingi. Miaka michache iliopita mji huo ulikuwa na matawi manne tu ya benki wakati 2011 tayari kulikuwa na matawi ya benki 15. Wakaazi wa hapo wanapenda kusema kwa dhihaka kwamba leo huko Tete kuna benki nyingi kuliko hata bekari za mikate, kuliko maduka ya madawa na kuliko hata maduka ya mboga mboga. Ingawa huko ni kutia chumvi lakini inadhihirisha kwamba Tete imebadilika.

WER: Eingang vom Markt in Tete. Früher hat man in der Provinzhauptstadt weder viele Autos noch viele Motorräder auf den Straßen gesehen. WO: Markt “1. Mai” (“Mercado Primeiro de Maio”), Stadt Tete, Tete-Provinz, Mosambik WANN: Juli 2012 AUTOR: Marta Barroso
Hapo zamani magari na pikipiki yalikuwa machache huko Tete- hivi sasa yamejaaPicha: DW

Tete kwa jicho la mwanaharakati

Manuel Cataqueta mfanya kazi katika shirika lisilo la kiserikali la haki za binaadamu la "Liga" wakati alipohamia Tete mwaka 2001 mji huo ulikuwa hauna kitu ziada ya kuwa kituo cha kusimama kwa muda kwa magari makubwa ya mizigo yaliokuwa yakipeleka bidhaa katika nchi jirani ya Malawi. Catequeta daima amekuwa akishangaa jinsi majengo mapya yanavyochipuka kila leo katika barabara kuu ya mji huo. Amekaririwa akisema kwamba "Hili jengo halifiki hata mwaka, zamani hapa ilikuwa ni sehemu ya jaa la taka. Sehemu nyingi za majaa ya zamani sasa kuna nyumba mpya. Hapo mbele tu kuna duka kubwa la bidhaa mbalimbali pia halifiki hata mwaka mmoja tokea kujengwa kwake."

Biashara ya nyumba inanawiri hapo Tete kwa kulinganisha na biashara nyenginezo. Catequeta anasema mwenye fedha za kununuwa ardhi, kujenga nyumba za kukodisha, maduka na ofisi anaweza kuishi raha mustarehe katika mji huo. Wakati alipohamia katika mji huo kodi ya nyumba nzuri ilikuwa ni euro 200 kwa mwezi lakini sasa inafikia hata euro 4,000.

Kwa mujibu wa mwanaharakati huyo leo kila mtu huko Tete ana simu ya mkononi na wale waliokuwa bado hawana wanataka kuwa nazo. Hadi hivi karibuni tu lilikuwa ni jambo lisilowezekana kununuwa simu za mkononi katika jimbo hilo. Madereva wa magari makubwa ya mizigo wamekuwa wakizipeleka simu hizo na hivi sasa kuna aina mbalimbali za simu hizo zinazopatikana hata kwenye soko la kienyeji ambalo pia huvutia watu kutoka mbali na hata kutoka nje ya nchi.

Wageni pia wavutiwa na Tete

Rohstoffprojekte in Afrika Kohleabbau in Mosambik Olivia. Sie ist Friseurin und Nagelkosmetikerin auf dem Zentralmarkt in Tete. Zwischen November 2009 und April 2010 wurden über 700 Familien vom brasilianischen Bergbauunternehmen Vale zwangsumsiedelt. Dafür hat der zweitgrößte Konzern im Bergbaubereich viele Versprechen gemacht, die bis heute nicht eingelöst wurden. Siedlung„Cateme“, Tete-Provinz, Mosambik, Juli 2012, Marta Barroso
Kwa fedha anazozipata Tete, Olivia hununua chakula na nguo kwa familia ilioko ZimbabwePicha: Marta Barroso

Olivia ana umri wa miaka 29. Yeye na shoga yake Faith wanafanya kazi ya kutengeneza nywele na kutengeneza makucha katika soko hilo. Miaka michache iliopita soko hilo lilikuwa na ukumbi mmoja tu unaouza mboga, matunda na nyama lakini sasa soko hilo limetanuka. Olivia na Faith wameingia Tete hapo mwaka 2008 kutoka nchi jirani ya Zimbabwe ambayo waliikimbia kutokana na kupanda kwa gharama za maisha nchini humo. Olivia anasema walisikia kwamba unaweza kujipatia fedha nzuri katika mji huo. Kwa maoni yake anasema "Tete inaendelea. Kuna kampuni nyingi zinazotoka Afrika Kusini na Amerika. Kampuni nyingi zinafunguliwa. Kuna majengo mengi yanayojengwa, wakati tulipokuja kulikuwa hakuna magari mengi sasa magari yamejaa barabarani. Mambo ni mazuri, wakati kampuni za kigeni zinapokuja Tete watu hufaidika kwa kupata ajira na kila kitu huboreka."

Kwa mujibu wa Olivia kwa siku anapata Meticais 500 hadi 1000 fedha za Msumbiji kama euro 15 hadi 25 na kwa kipato hicho anaweza kuishi vizuri. Wengi wanaolipwa vizuri huko Tete huwa wanatoka nchi za nje. Takriban vyakula vyote ambavyo kampuni huwanunulia wafanyakazi wake hutokea nchi jirani ya Afrika Kusini.

Umaskini bado kupungua

Rohstoffprojekte in Afrika Kohleabbau in Mosambik Alberto Vaquina. Bis Oktober 2012 war er Provinzgouverneur in Tete. Zwischen November 2009 und April 2010 wurden über 700 Familien vom brasilianischen Bergbauunternehmen Vale zwangsumsiedelt. Dafür hat der zweitgrößte Konzern im Bergbaubereich viele Versprechen gemacht, die bis heute nicht eingelöst wurden. Siedlung„Cateme“, Tete-Provinz, Mosambik, Juli 2012, Marta Barroso
Waziri Mkuu Alberto VaquinaPicha: Marta Barroso

Katika Repoti ya Umoja wa Mataifa ya Orodha ya Maendeleo ya Kibinaadamu, Msumbiji iko katika nafasi 184 kama ilivyokuwa hapo mwanzo kwa hiyo ni mojawapo ya nchi zenye kushikilia mkia. Burundi, Niger na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo bado zinaendelea kuwa na maendeleo duni. Hata kama uchumi wa Msumbiji unakua kwa asilimia saba kwa mwaka, idadi ya maskini haipunguwi. Uwekezaji kutoka nje unawekwa kwenye sekta ya malighafi tu kama ilivyo kwa kesi ya Tete. Miradi mikubwa kama wa makaa ya mawe wa Moatize inafaidika kutokana na kupunguziwa kodi. Hadi mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba mwaka 2012 Alberto Vaquina alikuwa ni gavana wa jimbo la Tete. Sasa amepandishwa cheo na kuwa Waziri Mkuu wa Msumbiji na anasema hafahamu kwa nini serikali isishughulikie suala la haki ya kugawana utajiri mpya wa nchi hiyo.

Anasema kila mwananchi atafute njia zake mwenyewe binafsi za kufaidika na neema hiyo ya malighafi. Kwa mujibu wa Vaquina lazima waendane na hali ya mambo ilivyo na kila mtu lazima apiganie ukombozi wake. Anaendelea kusema kwamba "Inamaanisha lazima nitafute njia ya kuishi kwa utu, kwa kutumia maarifa yangu, nguvu zangu na sio kutegemea kampuni." Kujikomboa zaidi kunamaanisha kupunguza utegemezi, kwa familia nyingi ambapo makaa ya mawe yamegunduliwa chini ya nyumba zao. Hata hivyo, kauli yake hiyo imeonekana kama ni dharao!

Vale yashindwa kutimiza ahadi

Rohstoffprojekte in Afrika Kohleabbau in Mosambik Zelte in der Siedlung „Cateme“. Zwischen November 2009 und April 2010 wurden über 700 Familien vom brasilianischen Bergbauunternehmen Vale zwangsumsiedelt. Dafür hat der zweitgrößte Konzern im Bergbaubereich viele Versprechen gemacht, die bis heute nicht eingelöst wurden. Siedlung„Cateme“, Tete-Provinz, Mosambik, Juli 2012, Marta Barroso
Wakaazi wa Cateme wanapaswa kuhamia kwenye mahemaPicha: Marta Barroso

Kati ya mwishoni mwa mwaka 2009 na mwanzoni mwa mwaka 2011 mamia ya wananchi hao walihamishwa kwa nguvu ambapo badala yake kampuni ya Vale ikatowa ahadi kubwa kwamba itatowa nyumba mpya, ajira mpya, shule mpya, hospitali na chakula bure. Hadi hii leo hakuna hata ahadi moja iliotimizwa. Familia hizo hivi sasa zinaishi kwenye kijiji kidogo cha Cateme kama kilomita 40 kutoka mahala walikozaliwa huko Moatize ambako walikuwepo hapo zamani. Baadhi ya wananchi walipigwa na kukamatwa na polisi wakati wa maandamano wakipinga hali hiyo. Miongoni mwao ni Gomes Antonio wa Shirika la haki za binaadamu la "Liga" juu ya kwamba hakushiriki maandamano hayo.

Tarehe 10 Januari mwaka 2012 mamia ya wakaazi wa Catema waliifunga njia ya reli iliokuwa ikitumika kusafirisha makaa ya mawe kutoka mgodi wa Moatize kuelekea bandari ya Moatize. Walitaka haki zao zizingatiwe na kampuni ya Vale itimize ahadi zake. Akilalamika, Gomes anasema "Kampuni ya Vale iliahidi kwamba tungeliweza kufanya kazi katika kampuni yake ya ujenzi kwa miaka mingi lakini hivyo sivyo ilivyo. Pia wametuahidi hekta mbili za ardhi lakina tumepewa moja tu. Njia iliokuwa inaelekea barabara kuu likuwa itiwe lami lakini hilo halikufanyika. Sio kila mtu ana umeme kama walivyoahidi. Chakula tulichokuwa tupewe kwa miaka mitano tumepewa kwa mwaka mmoja tu." Pia hata nyumba mpya zilizojengwa huko Cateme tokea mwanzo kabisa zilikuwa haziko katika hali nzuri kwani kuta zake zina nyufa na zinavuja.

2012_10_19_guinea_conakry_bauxit.psd

Tokea mwaka 2007 inatajwa kuwa kampuni ya Vale imefanya biashara ya takriban euro bilioni moja na kampuni za ndani ya nchi ikiwemo kampuni kubwa kabisa ya ujenzi nchini humo ya CETA iliopewa kandarasi ya kuzifanyia ukarabati nyumba za Cateme. CETA ni kampuni tanzu ambapo mwenye hisa kubwa ni Rais wa Msumbiji Armando Guebuza.

Hapo mwaka 2012 kampuni hiyo ya Vale imetajwa na shirika la kutetea mazingira duniani la Greenpeace kuwa ni kampuni mbaya kabisa ya mwaka ambapo wale wanaorambaza kwenye mitandao walitakiwa kupiga kura katika uchaguzi huo na ingelikuwa wakaazi wa Cateme wana mawasiliano ya mtandao sauti ya kuishutumu kampuni hiyo ingelikuwa kubwa zaidi.

Mwandishi: Marta Barroso/ Mohamed Dahman

Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman