1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makadirio mabaya ya kiuchumi

Oumilkher Hamidou18 Desemba 2008

Mzozo wa fedha watishia kuathiri ukuaji wa kiuchumi

https://p.dw.com/p/GIZv
Picha: picture-alliance / chromorange



Makadirio mabaya ya kiuchumi,shauri la kansela la kutaka vitega uchumi viingizwe pia katika sehemu ya magharibi ya Ujerumani na mpango wa kutumwa kikosi cha jeshi la wanamaji la Ujerumani katika fukwe za Somalia ni miongoni mwa mada zilizomulikwa zaidi na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.


Tuanze lakini na juhudi za kuwaandama maharamia wa kisomali.Gazeti la BRAUNSCHWEIGER ZEITUNG linaandika:


" Ndio, azimio la umoja wa mataifa linahalalisha kutumwa wanamaji.Suala lakini linalozuka ni jee maharamia wapelekwe wapi,pindi ikiwezekana kuwakamata? Na kama meli iliyotekwa nyara ni ya kijerumani ndo kusema maharamia hao wafikishwe mahakamani humu nchini?Kufanya hivyo haitakua haki hata kidogo.Lakini hata kuwafungulia kesi katika nchi walikotokea,si jambo linaloingia akilini.Tatizo hili linabidi haraka lipatiwe ufumbuzi.Ni vizuri kuona kwamba opereshini ya Atalanta imepamngiwa kwanza kudumu mwaka mmoja tuu."


Na gazeti la "NEUE OSNABRÜCKER ZEITUNG linachambua


Pale waziri wa mambo ya nchi za nje anapozungumzia juu ya kile ambacho wanamaji hawatakifanya-kwa mfano kuwaandama maharamia mpaka nchini Somalia kwenyewe,kama ilivyotajwa katika azimio la Umoja wa mataifa,anawagutua tuu  wahalifu wakadirie ipasavyo hatari wanayoweza kukabiliana nayo.Na hapo hasa ndipo kishindo chenyewe kilipo:maharamia wa kisomali,si magaidi,ni wafanya biashara werevu,waliotulia kabisa,wanaofuata mbinu wanazoamini zitawaletea faida.Bila ya shaka si kwa kutumia ndege kuiripua miji ya bandari au kujiingiza katika vita vya koo nchini humo.Bali kwa ujasiri kama walivyofanya wafaransa walipowashinda nguvu wale walioiteka nyara yoti ya anasa-"Le Ponant" mwezi April mwaka huu.Mbinu kama hizo zinawaonyesha maharamia jinsi mambo yanavyoweza haraka kuwageukia.



Mada ya pili magazetini inahusu makadirio mabaya ya kiuchumi nchini Ujerumani.Gazeti la BADISCHE NEUESTE NACHRICHTEN la mjini Karlsruhe linaandika:


Wenye kuashiria mabaya ndio wanaohanikiza hivi sasa.Mkuu wa masuala ya kiuchumi katika benki mashuhuri ya Ujerumani Deutsche Bank,Norbert Walter alikadiria hivi karibuni shughuli za kiuchumi zitaporomoka kwa asili mia nne mwakani.Inatia moyo kuona kwamba mkubwa wake mwenyewe,yaani Joseph Ackermann,amekosea alipohoji hivi karibuni eti mzozo wa kiuchumi utamalizika hivi karibuni.Waziri wa uchumi Michael Glos haondoi uwezekano kuoona uchumi wa Ujerumani ukiporomoka hadi asili mia tatu-kwamba makadirio hayo yanatolewa na waziri wa uchumi,ni ushahidi tosha wa picha ya wapiga chuku.