1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makamu wa rais Guinea ya Ikweta ahukumiwa nchini Ufaransa

10 Februari 2020

Mahakama ya rufaa ya mjini Paris Ufaransa imethibitisha hukumu ya kifungo cha nje cha miaka mitatu dhidi ya makamu wa rais wa Guinea ya Ikweta Theodorin Obiang, ambaye alituhumiwa kwa utakatishaji fedha.

https://p.dw.com/p/3XYyh
Äquatorialguinea Geburstag Teodorin Obiang
Picha: Getty Images/AFP/J. Leroy

Mahakama hiyo pia imemuamuru Obiang ambae ni mwanae wa kiume wa rais Theodore Obiang, kulipa faini ya euro milioni 30, ambayo ilikuwa imefutwa katika hukumu ya awali.

Mahakama ya rufaa ya mjini Paris imethibitisha uamuzi wa mahakama wa uhaini ya jiji hilo uliotolewa Oktoba mwaka 2017.

Theodorin Obiang ambae ni mwanae wa kiume wa rais Theodore Obiang, amekutwa na hatia ya kujitajirisha kwa njia zisizo halali. Huku akijirundikia fedha nchini Ufaransa pamoja na kumiliki makaazi ya kifahari nchini humo.

Kesi yake ilioitwa ''Biens Mal Acquis'' iliendesha kwa kipindi cha miaka miwili na mahakama ya rufaa nchini Ufaranza baada ya mawakili wa mushtakiwa kukata rufaa ya uamzi wa awali oktoba mwaka 2017.

Uamuzi umetolewa bila ya Theodorin kuwepo mahakamani

Uamuzi huo umekuja siku tatu baada ya kufunguliwa kwa kesi nyingine inayomuhusisha mwanae rais Dennis Sassou Ngouesso wa Congo -Brazzaville kwa makosa ya aina hiyo hiyo. Dennis Christel Sassou, mwenye umri wa miaka 45 amefunguliwa kesi kwa kuhusika na kutakatisha fedha.

Mbunge huyo wa jimbo la Oyo, kaskazini mwa Congo-Brazzaville, jimbo alikotokea baba yake alikuwa hadi mwaka 2006 akiongoza kampuni ya kitaifa ya mafuta.

Theodorin Obiang ambae ni mwanae wa kiume wa rais Theodore Obiang, amekutwa na hatia ya kujitajirisha kwa njia zisizo halali.
Theodorin Obiang ambae ni mwanae wa kiume wa rais Theodore Obiang, amekutwa na hatia ya kujitajirisha kwa njia zisizo halali.Picha: Getty Images/AFP/E. Feferberg

Kwenye ripoti iliotolewa mwezi Agosti mwaka jana , shirika la Uingereyza la Global Witness lilimtuhumu  Christel Sassou kwa kubadhiri dola milioni 50 za umma mnamo mwaka wa 2014. Ma bwana Theodorin Obiang na Denis Christel wote watoto wa marais walishitakiwa nchini Ufaransa na mashirika ya kiraia ya nchi yzao pamoja na mashirika ya kimataifa mfano wa Global Witness na Transpereancy International kwa ubadhirifu wa fedha za umma na utakatishwaji wa fedha.

Kesi yake pia ilihusisha baadhi ya familia za marais wa Gabon na Congo-Brazzaville

Majumba kadhaa ya kifahari, zikiwemo mbili yza Antoinette Sassou Nguessso, mke wa rais wa Congo-Brazzaville yalizuwiliwa na mahakama ya Ufaransa. Kesi hizo za ''Biens mal Acquis'' zilifunguliwa toka mwaka wa 2009, na zimehusisha familia za marais wa Gabon  Ali Bongo, wa Equatorial Guinea Theodore Obiang Nguema na Congo-Brazzaville Denis Sassounguesso.

Mwaka 2016, rais Sassou Nguesso alilishitaki shirika la Transparency International kwa kile alichoelezea kuwa ni kukashifu jina lake.

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya rufaa mjini Paris amesema kwamba familia za marais hao zinamiliki baadhi ya makaazi na fedha kwenye benki kadhaa nchini Ufaransa.

Mwandishi: / Saleh Mwanamilongo/AFPF

Mhariri: Daniel Gakuba