1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran sasa itaondolewa vikwazo ilivyowekewa

19 Oktoba 2015

Marekani pamoja na Umoja wa Ulaya zitaanza kujitayarisha kuviondoa vikwazo vya kibiashara vilivyoudhoofisha uchumi wa Iran, huku makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran yakianza kutekelezwa leo hii.

https://p.dw.com/p/1GqM6
Federica Mogherini und Mohammad Javad Zarif Iran
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini akiwa na Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa IranPicha: Mehr

Utaratibu wa kuiondolea Iran vikwazo hivyo unaanza siku 90 baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha makubaliano hayo kwa kutia saini mjini Vienna mwezi Julai, na inayojulikana kama "Siku ya utekelezaji".

Hata hivyo mashirika ya kigeni hayatoweza kurejesha mahusiano ya kibiashara na sekta ya mafuta ya Iran pamoja na mabenki kwa sasa -- vikwazo hivyo bado vitabaki kuwapo hadi pale Iran itakapotimiza majukumu yake iliyoahidi wakati wa mapatano.

Hatua itakayofuatia katika mchakato huu -- siku ya utekelezaji -- itakuja pale wakaguzi wa masuala ya nuklia wa Umoja wa Mataifa wa Shirika la Kimataifa la kudhibiti Nishati ya Nuklia (IAEA), watakapothibitisha kwamba Iran imepunguza kwa kiasi kikubwa mpango wake wa kutengeneza silaha za nuklia.

Iran kwa upande wake imesema mchakato huo ambao unategemewa kuchukua muda, utaanza rasmi wiki hii.

Wajumbe kukutana Vienna

Leo hii, wajumbe wa nchi nchi zilizoshiriki na kuweka saini katika makubaliano ya mpango huwo wa nuklea ikiwamo ; Uingereza, Uchina, Ufaransa, Ujerumani, Urusi pamoja na Marekani – zitakutana mjini Vienna kuunda tume itakayosimamia utekelezaji wa makubaliano hayo.

Iran inatakiwa kusalimisha hifadhi yake ya mafuta ya kutengenezea silaha za nuklea, pamoja na kukongoa mtambo wake wakutengeneza kemikali za nuklea.

Hapo ndipo amri ya rais wa Marekani, Barack Obama, ya hivi karibuni ya kuodowa vikwazo dhidi ya Iran itakapotekelezwa na biashara pia itakaporejeshwa baina ya nchi hiyo mbili.

Barack Obama am Schreibtisch
Rais wa Marekani Barack ObamaPicha: picture-alliance/AP Photo/C. Dharapak

"Leo ni siku muhimu na tunapiga hatua mbele katika kuizuia Iran kutengeneza silaha za kinyuklia pamoja na kuhakikisha kwamba mpango wake wa kinyuklia utaendelea kuwa wa salama katika siku za mbele," alisema rais wa Marekani barack Obama katika taarifa yake ndani ya ikulu ya nchi hiyo - White House.

Maafisa waandamizi kadhaa waliozungumza na waandishi habari na waliokataa kutajwa kwa majina, wamesema kwamba vikwazo dhidi ya Iran vitaanza kuondolewa baada ya miezi miwili.

Umoja wa Ulaya nao umepitisha mfumo wa kisheria wa kuindolea vikwazo Iran.

"Mfumo huwo wa kisheria 'utawasaidia kupiga hatua mbele na kuwa ndio mwanzo wa kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa Julai iliyopita, ambayo sote tuna nia ya kuyatekeleza kwa dhati", alisema Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini, katika taarifa ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Javad Zarif.

Waziri wa fedha wa Marekani Jacob Lew amesema Iran ikiwa inajiandaa kuchukua hatua za kupunguza mpango wake wa Nuklea na huku Marekani pamoja na washirika wake wakiwa wanajitayarisha kuiondolea vikwazo Iran, tunachukua hatua moja mbele kufanikisha makubaliano yetu, pamoja na kuhakikisha kuwa tuna jumuiya ya kimataifa iliyo salama.

Vikwazo vengine vitabaki kuwapo

Hata hivyo Iran inakana kwamba mpamngo wake wa kinyuklia ulikuwa na lengo la kutengeneza silaha za kinyuklia.

Baadhi ya vikwazo ilivyoiwekea Iran na Marekani vitabaki kuwapo hata baada ya kutekelezwa makubaliano ya mpango wa nyuklia, ikiwamo vile vinavyohusika na ukiukwaji wa haki za binaadamu.

Mwandishi Yusra Buwayhid/rtre/afpe

Mhariri:Yusuf Saumu