1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MALE:Mlipuko wa bomu wajeruhi watalii 12

30 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLZ

Watu 12 wamejeruhiwa wengi wakiwa ni watalii kufuatia mlipuko wa bomu karibu na msikiti mmoja kwenye mji mkuu wa visiwa vya Maldives, Male.

Waliyojeruhiwa ni watalii kutoka , Japan, Uingereza na China ambapo maafisa wa serikali wamesema kuwa mpaka sasa hakuna mtu yoyote aliyedai kuhusika na shambulizi hilo.

Ni shambulizi la kwanza kukikumba kisiwa hicho cha Maldives chenye idadi kubwa ya waislam na ambacho ni maarufu kwa utalii.