1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mali yamtimua kocha wa taifa Kasperczak

9 Machi 2015

Mali imemwambia kwaheri kocha Henryk Kasperczak baada ya timu ya taifa kushindwa kufuzu katika raundi ya kwanza ya dimba la Kombe la Mataifa ya Afrika lililokamilika katika Guinea ya Ikweta.

https://p.dw.com/p/1EniF
Mali Fußball Nationalmannschaft
Picha: H. Kouyate/AFP/Getty Images

Hiyo ni mara ya pili ambapo timu ya taifa ya Mali imemtimua kocha huyo mwenye umri wa miaka 68, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Poland iliyoshiriki Kombe la Dunia.

Kasperczak aliifikisha Mali katika nafasi ya nne ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka wa 2002, ambalo walikuwa wenyeji, lakini katika kipindi chake cha pili cha uongozi, timu hiyo ilibanduliwa nje katika hatua ya kwanza katika dimba hilo nchini Guinea ya Ikweta.

Kasperczak amewahi pia kuwa mkufunzi wa Cote d'Ivoire, Morocco, Senegal na Tunisia na alishiriki katika vinyang'anyiro sita vya AFCON.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman