1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maliasili duniani itumiwe kwa uangalifu na heshima

25 Desemba 2009

Rais wa Ujerumani Horst Koehler ametoa mwito wa kuitumia kwa uangalifu zaidi maliasili ya dunia.

https://p.dw.com/p/LDHR
** SPERRFRIST Donnerstag, 24. Dezember 2009, 0:00 Uhr ** ** EMBARGOED UNTIL THURSDAY, DEC. 24, 2009, 0:00 CET ** Das am Dienstag, 22. Dezember 2009, vom Bundespresseamt zur Verfuegung gestellte Bild zeigt Bundespraesident Horst Koehler waehrend der Aufzeichnung der Weihnachtsansprache in seinem Arbeitszimmer im Schloss Bellevue in Berlin. (AP Photo/Bundesregierung) ** SPERRFRIST Donnerstag, 24. Dezember 2009, 0:00 Uhr ** ---- Picture provided by German government on Tuesday, Dec. 22, 2009 shows German President Horst Koehler during the taping of his Christmas speech. (AP Photo/German government) ** EMBARGOED UNTIL THURSDAY, DEC. 24, 2009, 0:00 CET **
Rais wa Ujerumani Horst Köhler akitoa hotuba ya Krismasi.Picha: AP

Katika hotuba aliyotoa mkesha wa Siku Kuu ya Krismasi Rais wa Ujerumani amesema,utaratibu wa kihaki duniani unapaswa pia kuambatanisha usimamizi bora zaidi katika sekta ya fedha.

Mara nyingine tena Rais Köhler amekosoa na kusema kuwa tamaa ya kubahatisha iliyopindukia ndio iliyosababisha msukosuko wa fedha wa hivi karibuni.

Vile vile amesifu kazi zinazofanywa na mamilioni ya raia wenye utambuzi wa kijamii na wanajeshi wa Kijerumani wanaoshiriki katika tume zilizoidhinishwa na Umoja wa Mataifa katika nchi za ngámbo.