1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malkia wa Uholanzi aruhusu serikali kuundwa.

8 Oktoba 2010

Malkia Beatrix wa Uholanzi amemruhusu kiongozi wa chama cha kihafidhina cha WD, Mark Rutte kuunda serikali ya wachache yenye kufuata mrengo wa kati kulia.

https://p.dw.com/p/PYyf
Kiongozi wa chama cha siasa cha VVD, nchini Uholanzi, Mark Rutte.Picha: picture-alliance/dpa

Serikali hiyo itaundwa kwa kushirikiana na chama cha Christian Democrats na pia kuungwa mkono bungeni katika masuala fulani, na chama cha mwanasiasa mbaguzi anayeupinga uislamu, cha Uhuru, Geert Wilders.

Mark Rutte Maxime Verhagen Geert Wilders NO FLASH
Kiongozi wa chama cha mrengo wa kati kulia nchini Uholanzi, Mark Rutte (kushoto), akiwa na kiongozi wa chama cha Christian Democrats, Maxime Verhagen (kati) na wa chama cha Uhuru Geert Wilders (kulia).Picha: picture-alliance/dpa

Kulingana na makubaliano hayo yaliyofikiwa wiki moja iliyopita, chama cha Wilders kitakuwemo katika baraza la mawaziri litakaloundwa, ambalo malkia amemtaka bwana Rutte kulishughulikia haraka iwezekanavyo.

Uholanzi imekuwa katika mzozo wa kisiasa tangu muungano uliokuwa madarakani, ambao ulikuwa ukiongozwa na Waziri mkuu Jan Peter Balkenende kuvunjika, Februari mwaka huu.

Rutte anatarajiwa kuongoza serikali ya kwanza ya wachache tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia.

Mwandishi: Halima Nyanza (zr)

Mhariri: Josephat Charo