1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia waandamana kupinga mkutano wa G8

5 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/EWq6

Toyako Japan

Mamia ya watu wanaandamana kaskazini mwa Japan kupinga mkutano wa kilele ujao wa kundi la nchi nane tajiri kiviwanda duniani la G8.Waandamanaji hao ni pamoja na makundi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali pamoja na makundi ya kiraia ambayo yanapinga kushindwa kwa mataifa hayo tajiri kupambana na umaskini na vita duniani..Akizungumzia kuhusu mkutano huo Kansela Anegla Merkel wa Ujerumani amependekeza hatua kadhaa zichukuliwe kupambana upungufu wa vyakula pamoja na kuanzishwa mikakati ya muda mrefu ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo duniani.Nchi hizo nane tajiri zitafanya mkutano wake wa kilele katika mji wa Toyako nchini Japan kuanzia tarehe 7 hadi 9