1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Man City taabani kuhusu Champions League

Admin.WagnerD10 Mei 2016

Manchester United ina kivutio cha kuwania kuingia katika nafasi ya kucheza katika Champions League wakati wakijitayarisha na pambano dhidi ya West Ham United

https://p.dw.com/p/1Iko0
Fußball Champions League Real Madrid CF - Manchester City
Picha: picture-alliance/AP Photo/F. Seco

Sare ya mabao 2-2 kati ya Manchester City na Arsenal jana Jumapili ina maana United inaweza kuwapiku mahasimu wao wa mtaani Manchester City na kuingia katika nafasi nne bora za kucheza Champions League msimu ujao iwapo itaishinda West Ham na kisha kuisambaratisha Bournemouth siku ya Jumapili.

Kocha anayeondoka kuifunza Manchester City Manuel Pellegrini amejitahidi kuonesha uso usio huzuni baada ya timu yake kujiweka katika nafasi ngumu kucheza katika Champions League msimu ujao. Lakini amesema "nadhani tunastahili kuwamo katika Champions League msimu ujao kwasababu tulikuwa na michezo 37 katika nafasi ya Champions League, kwa hiyo sidhani kama tutaipoteza nafasi hiyo katika mchezo wa mwisho.

England Fußball Manchester United vs. Leicester City
Man United wana nafasi nzuri ya kucheza Champions LeaguePicha: Reuters/J. Cairnduff

Hata hivyo Manchester City inategemea tu kuwamo katika kinyang'anyiro hicho iwapo mahasimu wao Manchester United watapoteza pointi katika michezo yao mwili ya mwisho.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amefuta wito wake kwa mashabiki wa Liverpool ambao hawatakuwa na tikiti kwa ajili ya mchezo wa fainali ya kombe la ligi ya Ulaya Europa League kwenda mjini Basel Uswisi kuangalia pambano hilo la fainali dhidi ya Sevilla hapo Mei 18, na kusema anajuta kutoa taarifa hiyo.

Liverpool imepewa nafasi 10,000 tu kwa mashabiki wao kwa ajili ya mchezo huo wa fainali lakini Klopp aliwataka mashabiki kwenda mjini Basel hata kama hawana tikiti, na kusababisha shirikisho la soka la Ulaya EUFA kuwaonya mashabiki ambao hawatakuwa na tikiti kujiweka mbali na uwanja huo utakaofanyika fainali.

Ubingwa wa La liga wasubiriwa

Na huko Uhispania ubingwa unasubiriwa hadi mchezo wa mwisho, na hali hii imezoeleka , ambapo timu mbili zinakodolea macho ubingwa, wakati Barcelona ikiwa mbele na mahasimu wao wakubwa Real Madrid ikiwa nyuma yao.

Barca inahitaji ushindi kuweka kusajili ushindi wao wa 24 kufuatia ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Espanyol Barcelona.

Real wako nyuma pointi moja baada ya kuishinda Valencia kwa mabao 3-2. Iwapo Barcelona timu hizo zitamaliza zikiwa pointi sawa, Barca itaibuka kidedea kutokana na kuwa mbele wakati wote wa ligi hiyo, lakini iwapo Barca itashindwa kupata ushindi dhidi ya Granada wiki hii kikosi cha Zinedine Zidane kinaweza kutawazwa mabingwa kwa ushindi dhidi ya Deportivo La Coruna.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe / dpae
Mhariri: Iddi sessanga