1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mancini amkunja shati Balotelli

3 Januari 2013

Hatma ya mchezaji wa Manchester City Mario Balotelli imeingia ukungu kwa mara nyingine tena baada ya picha kuibuka zikimuonesha katika mvutano wakati wa mazowezi na kocha wake Roberto Mancini.

https://p.dw.com/p/17DBe
Italy's Mario Balotelli celebrates scoring his side's second goal during the Euro 2012 soccer championship semifinal match between Germany and Italy in Warsaw, Poland, Thursday, June 28, 2012. (Foto:Vadim Ghirda/AP/dapd)
Mario Balotelli alikunjana ngumu na kocha wake ManciniPicha: AP

Ripoti za vyombo vya habari zinadai kuwa Manicini alijawa na jazba dhidi ya raia mwenzake huyo Mtaliani baada ya Balotelli kumkaba kwa njia isiyopendeza mchezaji mwenzake Scott Sinclair katika uwanja wa mazowezi wa timu hiyo nje kidogo ya mji wa Manchester.

Picha , zilizochapishwa na vyombo kadha vya habari nchini Uingereza , zinamuonesha Mancini akimkunja shati Balotelli akiwa na hasira nyingi, kabla ya watu hao wawili kutenganishwa na baadhi ya wafanyakati wa benchi la ufundi la Manchester City.

Manchester City's new Bosnian striker Edin Dzeko, right, poses for photographs with his manager Roberto Mancini at the club's Carrington training ground, Manchester, England, Tuesday Jan. 11, 2011. (Foto:Jon Super/AP/dapd)
Kocha Roberto Mancini Flash- wa ManchesterPicha: dapd

Mtu aliyeshuhudia , alinukuliwa na gazeti la Uingereza la Manchester Evening News, akisema, "Mancini alikimbia hadi kwa Balotelli na alikuwa amekasirika sana. Alimkunja shati na alionekana akitaka kumwangusha chini.

"Inaonekana kama Mario alikuwa na nguvu mno na hakuweza kumwangusha. Baadaye makocha wote walikimbia kuwatenganisha lakini Mancini alikuwa hakubali. Aliendelea kujaribu aachiliwe na kupambana na Baloteli tena."

Balotelli pia alipigwa picha akijaribu kwenda katika eneo la kuegesha magari baada ya kumalizika kipindi cha mazowezi.

Mshambuliaji huyo wa Italia , mwenye umri wa miaka 22 amekuwa chanzo cha utata tangu kuwasili Manchester akitokea Inter Milan mwaka 2010.

Chelsea yasema na Ba

Wakati huo huo Chelsea imepewa nafasi ya kuzungumza na mshambuliaji wa Newcastle United Demba Ba baada ya kutoa ombi ambalo limezusha kuwapo kwa kifungu cha mchezaji huyo kuweza kuondoka katika klabu hiyo katika mkataba wake, imethibitisha timu hiyo ya Newcastle.

Hoffenheim's Demba Ba celebrates after scoring the first goal for his team during the German first division Bundesliga soccer match between Hertha BSC Berlin and TSG 1899 Hoffenheim in Berlin, Germany, Saturday, Feb, 27, 2010. (apn Photo/Kai-Uwe Knoth) **NO MOBILE USE UNTIL 2 HOURS AFTER THE MATCH, WEBSITE USERS ARE OBLIGED TO COMPLY WITH DFL-RESTRICTIONS, SEE INSTRUCTIONS FOR DETAILS**
Mshambuliaji kutoka Senegal Demba BaPicha: AP

Chelsea inaweza kuanza mazungumzo na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Senegal baada ya kukubali kulipa kitita cha pauni za Uingereza milioni 7, sawa na euro milioni 8.6, kama inavyoelezwa katika mkataba wake.

Ba ambaye alijiunga na Newcastle mwaka 2011, akitokea Hoffenheim ya Ujerumani , aliondolewa katika kikosi cha kocha Alan Pardew ambacho kilipata kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Everton Jumatano jioni.

Mlinzi wa timu ya taifa ya Uingereza Phil Jagielka ametia saini kurefusha mkataba wake wa sasa na Everton, na kumfunga na klabu hiyo hadi majira ya joto 2017.

Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 30 bado ana miaka miwili na nusu kabla ya mkataba wake kumalizika , lakini aliamua kurefusha mkataba wake na klabu hiyo iliyoko chini ya uongozi wa David Moyes.

Valdes huenda akahama Barca

Mlinda mlango wa Barcelona Victor Valdes amefungua mlango wa uwezekano wa kuhamia nje ya Uhispania wakati mkataba wake utakapomalizika na viongozi wa ligi ya nchi hiyo La Liga mwishoni mwa msimu ujao.

Barcelona's goalkeeper Victor Valdes, reacts while receiving a yellow card during his Spanish La Liga soccer match against Barcelona at the Santiago Bernabeu stadium in Madrid, Saturday, April 16, 2011. (AP Photo/Arturo Rodriguez)
Victor Valdes wa BarcelonaPicha: AP

Valdes , kipa namba mbili wa timu ya taifa ya Uhispania nyuma ya Iker Casillas, atakuwa na umri wa miaka 31 mwezi huu na amekuwa Barcelona tangu alipojiunga nayo katika academy ya klabu hiyo mwaka 1995, na kuanza kuichezea timu ya kwanza katika msimu wa mwaka 2002-03.

Walinzi wa Arsenal London Sebastien Squillaci na Johan Djourou huenda wakaihama timu hiyo katika dirisha dogo la mwezi huu, ameeleza kocha wa Arsenal , Arsene Wenger katika tovuti ya klabu hiyo.

Wachezaji hao wawili wamekuwa wakisumbuka kuweza kuingia katika kikosi cha kwanza. Mchezaji wa timu ya taifa ya Uswisi Djourou mwenye umri wa miaka 25 amecheza mara mbili tu msimu huu na mchezaji wa Ufaransa Squillaci , mwenye umri wa miaka 32 amecheza mara moja tu.

Cruyff asema basi

Kocha wa zamani wa Ajax na Barcelona Johan Cruyff amedokeza kuwa muda wake wa kuwa kocha huenda umekwisha baada ya kuiongoza timu ya kombaini ya Catalonia katika sare ya bao 1-1 dhidi ya nigeria jana.

Johan Cruyff, the Dutch great who once coached Barcelona Club, pauses during his presentation as the new advisor for the Chivas de Guadalajara team at the Omnilife stadium in Guadalajara, Mexico, Saturday Feb. 25, 2012. 2012. Cruyff, 64, was introduced at a new conference where the team owner said Cruyff received a three-year contract and would be visiting the club several times each year to oversee all facets of team development from the youth system to the first team.(Foto:Bruno Gonzalez/AP/dapd)
Johan CruyffPicha: AP

Cruyff alianza ukocha baada ya kucheza kwa ufanisi nchini mwake Uholanzi akiwa na timu ya Ajax na Uhispania akiwa na Barcelona na ni mmoja kati ya watu wanne pamoja na Michel Platini , Marco van Basten na Lionel Messi kushinda mara tatu tuzo ya mchezaji bora wa dunia.

Mwandishi : Sekione Kitojo/ dpae / rtre / afpe