1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Demokrasia dhaifu Afrika

Claus Staecker21 Machi 2016

Habari kuhusu Cuba, ugaidi na wakimbizi zimefudikiza zile za Jumapili Kabambe Afrika ambapo nchi tano zilifanya uchaguzi na kudhihirisha udhaifu wa demokrasia barani humo anaandika Claus Staecker.

https://p.dw.com/p/1IH8s
Wanajeshi wa Jamhuri ya Congo na raia wakiwa katika mstari kupiga kura mjini Brazaville. (20.03.2016)
Wanajeshi wa Jamhuri ya Congo na raia wakiwa katika mstari kupiga kura mjini Brazaville. (20.03.2016)Picha: picture-alliance/AP Photo/J. Bompengo

Mwishoni mwa juma kulikuwa na uchaguzi katika nchi tano tafauti za Afrika - Benin, Cape Verde, Niger, Jamhuri ya Congo na Zanzibar na zote hizo zinaonyesha jinsi demokrasia ilivyo rahisi kudhurika barani Afrika

Kwa kadri suala la uwazi katika demokrasia ya vyama vingi barani Afrika bado kabisa sio suala la kupigiwa mfano. Miamba miwili ya demokrasia wa bara hilo tayari imeangushwa kwa urahisi. Kisiwa cha Cape Verde kilikuwa kimo katika nafasi tano za juu katika kipimo cha demokrasia.

Faharasa ya Mo Ibrahim imeiweka nchi hiyo katika nafasi ya pili. Ripoti kuhusu uhuru duniani umeiweka nchi hiyo katika nafasi ya nne miongoni mwa nchi zenye uhuru mkubwa duniani.Kwa hiyo sio jambo la kushangaza kwa waziri mkuu anatimiza wajibu wake kwa mujibu wa katiba na kwa hiari katika koloni hilo la zamani la Ureno baada ya chama chake cha PAICV kushindwa katika uchaguzi.

Chama hicho kilikuwa na mgombea mpya mwanamke mwenye umri wa miaka 37 kuwania wadhifa huo jambo ambalo ni la kupigiwa mfano barani Afrika ambapo wanaume takriban ndio wanaohodhi madaraka.

Claus Staecker, mkuu wa idara ya Afrika ya DW.
Claus Staecker, mkuu wa idara ya Afrika ya DW.

Lakini ujana wa Janira Hopffer Almanda umeshindwa kuwavutia wapiga kura.Hiyo ndio demokrasia. Mgombea wa chama cha kihafidhina Correia da Silva alishinda kwa sababu wapiga kura walikuwa na imani kwamba anaweza kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kichumi ya nchi hiyo.Kwa vyo vyote vile ameahidi ajira mpya 45,000

Huko Benin Afrika Magharibi Rais Boni Yayi amen'gatuka kwa hiari baada ya kutumikia mihula miwili madarakani. Lakini mtu wa kuchukuwa nafasi yake sio mgombea wa chama tawala FCBE yaani Waziri Mkuu Lionel Zinsou bali ni mgombea wa upinzani Patrice Lionel Talon ambaye alikuwa mfanya biashara wa pamba na meneja kwa mamilioni ya wafanyakazi wa bandari. Wapiga kura walikuwa wakitaka mabadiliko licha ya kujitokeza kwa idadi ndogo ya wapiga kura na umashuhuri wa Talon kutokuwa mkubwa kiasi hicho.

Tafauti na uchaguzi katika Jamhuri ya Congo Rais Sassou Ngueso hafikirii kabisa suala la kun'gatuka licha ya kuwa madarakani kwa miaka 32. Baada ya kura ya maoni hapo mwezi wa Oktoba mwaka 2015 ambayo upinzani unaiona kuwa yalikuwa mapinduzi ya katiba vifungu vyote viwili kile cha kikomo cha mihula miwili na umri usiopindukia miaka sabini vilifutwa kumuwezesha kiongozi huyo kuwania tena. Nguesso ana umri waiaka 72.

Katika visiwa vya Zanzibar vyenye mamlaka yake ya ndani nchini Tanzania chama tawala cha CCM kimeendelea kun'gan'gania madaraka.

Upinzani na vyombo vya habari vilitishwa na kusumbuliwa kabla ya uchaguzi huo akiwemo mwandishi wa Deutsche Welle, Salma Said.

Baada ya chama kikuu cha upinzani cha CUF kuususia uchaguzi huo CCM ambayo inatawala Tanzania bara pia itaendeleza utawala wake Zanzibar kwa ushindi wa rais unaotwajwa kupindukia asilimia 91. Kutekwa na watu wasiojulikana kwa siku mbili na nusu kwa mwandishi huyo wa Deitshe Welle kuliamsha mshikamano wa taifa zima.Rais John Magufuli wa Tanzania ambaye amekuwa mfano wa kuigwa katika kupambana na rushwa barani Afrika anakabiliwa na changanoto kubwa ya kuidhibiti CCM Zanzibar ilio na ukaidi.

Nchini Niger tangazo la ushindi wa rais aliyekuwa akitetea kiti chake Issofou Mahamadou ulikuwa kama ni kutimiza desturi kwa sababu upinzani ulisusia uchaguzi huo wa marudio.Mpinzani wake Hama Amadou aliondolewa nchini humo moja kwa moja kutoka gerezani kwenda kupatiwa matibabu nchini Ufaransa. Taifa hilo liko katika mapambano na kundi la Al Qaeda na Boko Haram na limepiga hatua kubwa katika kuwania demokrasia na uhuru wa kujieleza katika miaka ya hivi karibuni.

Mizizi ya demokrasia ni dhaifu takriban kila mahala barani humo.Uchaguzi wenye mafanikio hauhahakikishi makabidhiano ya madaraka kwa utulivu katika demokrasia ya vyama vingi barani Afrika.

Mwandishi: Claus Staecker /Mohamed Dahman
Mhariri: Yusuf Saumu