1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Hakuna matumaini Congo

26 Novemba 2012

Hakuna ishara ya kumalizika mzozo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako sio tu kundi la waasi M23, bali hata makundi mengine ya waasi na wanajeshi wa serikali wanavunja haki za binaadamu kila siku.

https://p.dw.com/p/16oyN
Congolese flees the eastern Congolese town of Sake , 27kms west of Goma, Friday Nov. 23 2012. Thousands fled the M23 controlled town as platoons of rebels were making their way across the hills from Sake to the next major town of Minova, where the Congolese army was believed to be regrouping. The militants seeking to overthrow the government vowed to push forward despite mounting international pressure.(Foto:Jerome Delay/AP/dapd)
Wakimbizi nchini DRCPicha: AP

Pamoja na waasi wa M23, kuna makundi mengine ya waasi na wanamgambo katika eneo la mashariki la nchi hiyo yanayofanya maovu, wanapora mali, wanawabaka watu na wanauwa. Wanaosumbuliwa ni raia wa kawaida wasiokuwa na kinga yoyote. Ndiyo kusema hakuna hamu ya kupatikana amani ya kweli nchini Congo? Ndiyo kusema jumuiya ya kimataifa imeshindwa kutokana na matatizo ya kila aina ya nchi hiyo ya Afrika Kati?

Katika eneo la mashariki la Congo kuna vurugu. Mwenye nguvu za kijeshi ndie mshindi. Wananchi wa kawaida wanajikuta wakikumbwa na mashambulio bila ya kuwa na kinga yoyote. Hawana njia nyengine isipokuwa kufuata majaaliwa yao. Jumuia ya kimataifa itakodoa macho mpaka lini? Wangapi wanabidi wapoteze maisha yao katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, wanawake wangapi, wasichana wangapi, mabibi watuwazima na hivi sasa hata wanaume wanabakwa, hadi jumuia ya kimataifa itakapoamua kuimarisha juhudi zao za kusaka amani katika eneo hilo la mzozo na kutathmini upya mkakati uliokuwa ukitumika hadi sasa?

Rais Kabila hana nguvu za kuongoza

Ukweli ni kwamba kuna serikali katika jamhuri ya kidemokrasi. Ukweli lakini pia ni kwamba hakuna kinachotendeka nchini humo. Rais Joseph Kabila hana nguvu zozote za kuiongoza nchi hiyo ambayo kimsingi iko katika ramani tu .Katika sehemu kubwa ya nchi hiyo hakuna sheria, hakuna polisi wala miundo mbinu yoyote ya serikali. Mara nyingi jeshi linajikuta likipora mali ili kuweza kuyanusuru maisha yao kwasababu wanajeshi mara nyingi wanapitisha miezi bila ya kulipwa mishahara. Makamanda wanawauzia waasi na wahalifu silaha zao. Baada ya Goma kuangukia mikononi mwa kundi la waasi la M23, wanajeshi waliokuwa katika eneo hilo, hawakutaka kupigana, walijiunga moja kwa moja na waasi.

epa03029391 (FILE) A file picture dated 24 October 2011 shows Joseph Kabila, President of the Democratic Republic of Congo, looking on, during the closing news conference at the Francophone Summit in Montreux, Switzerland. Incumbent Joseph Kabila was on 09 December 2011 declared the winner of last month's presidential elections in the Democratic Republic of Congo, defeating 10 other candidates, according to the country's election commission. The results still need to be confirmed by the supreme court. According to media reports on 09 December 2011, opposition leader Etienne Tshisekedi has declared himself president, only a few hours after hours after provisional results shows that Joseph Kabila had won. EPA/DOMINIC FAVRE *** Local Caption *** 00000402410042
Rais Joseph Kabila wa CongoPicha: picture-alliance/dpa

Si jambo linaloingia akilini kuona nchini Congo, hata katika karne hii ya 21,bado "mwenye nguvu ndiyo mwenye usemi." M23, sawa na makundi yote mengine ya waasi na yale yanayojiita ya wanamgambo hayana haki yoyote ya kutawala nchini Congo, kuwaamaulia mustaakbal wao raia au hata kujinata kama "waokozi" wa wananchi.

MONUSCO wachukiwa na raia

Wanajeshi 17.000 wa vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda amani nchini Congo, MONUSCO idadi kubwa kabisa kuwahi kutumwa na Umoja wa mataifa ulimwenguni, kwa miaka sasa wamekuwa wakikosolewa kwamba hawana lao. Wanajeshi wa umoja wa mataifa wanachukiwa na idadi kubwa ya wananchi, wanahisi hawajawahami. Zaidi ya hayo juhudi za tume hiyo ya Umoja wa Mataifa daima zimekuwa zikikorofishwa kutokana na ukosefu wa ushirikiano naiwe kwasababu ya kigeugeu au uzembe wa serikali ya rais Joseph Kabila.

A MONUSCO (the UN mission in Democratic Republic of Congo) soldier patrols in the deserted streets of Goma late on October 16, 2012. Amnesty International last week called on the Democratic Republic of Congo to put an end to the fighting in the east of the country where several local and foreign armed groups are committing abuses. AFP PHOTO / JUNIOR D. KANNAH (Photo credit should read JUNIOR D.KANNAH/AFP/Getty Images)
Vikosi vya MONUSCO, CongoPicha: D.KANNAH/AFP/Getty Images

Haisaidii kitu kwa hivyo mwito wa nia njema wa wanasiasa wa magharibi au maazimio ya Umoja wa Mataifa mfano wa lile la nambari 2076 lililopitishwa Novemba 20 mwaka huu ambapo kisa cha kutekwa mji wa Goma kililaaniwa na waasi kutakiwa waweke chini haraka silaha zao na kusalim amri.

Kwa upande wao wanazidi kusonga mbele. Haitoshi kuwaweka wakuu wa makundi hayo ya waasi katika orodha ya wanaosusiwa. Wanapuuza vikwazo vya umoja wa mataifa, na waasi wengi wanaonyesha hawajali hata kitisho cha kujikuta siku moja wakifikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu mjini The Hague.

Suala kwa hivyo linalozuka ni je, Jumuiya ya kimataifa inabidi ifanye nini ili kuzuwia uvunjwaji wa haki za binaadam na kukomesha mapigano yasiyokwisha mashariki ya Congo?

Vikosi vya MONUSCO vinalazimika kuwalinda wananchi wa kawaida. Madai hayo yametolewa pia hivi karibuni na mwaakilishi mkuu wa siasa ya nje wa Umoja wa Ulaya bibi Catherine Ashton mjini Brussels. Hadi wakati huu jukumu la vikosi hivyo lilikuwa la ushirikiano pamoja na jeshi. Kinatokea nini lakini ikiwa wanajeshi wenyewe wanakimbia. Ndio maana jukumu linabidi liambatane na hali halisi ya mambo katika eneo husika MONUSCO wapatiwe nguvu zinazohitajika pamoja na kuimarishwa ushirikiano kati ya Umoja wa mataifa na mashirika ya kimkoa.

Muhimu pia ni kuwepo mdahalo wa kitaifa. Shinikizo linabidi lizidishwe toka nchi jirani ili kuweza kukomesha hatimae misaada wanayopatiwa waasi. Kwamba hayo yanatendeka, imedhihirishwa katika ripioti ya hivi karibuni ya umoja wa mataifa. Pande zote zinabidi ziketi katika meza ya mazungumzo. Na mataifa fadhili yanabidi yazidishe shinikizo kwa Rais Kabila na serikali yake ya wala rushwa. Mashirika ya huduma za jamii yastahiki kuhusishwa katika juhudi za kuandaa mkakati madhubuti wa kuleta amani katika eneo la mashariki.

Haisaidii kitu kulalamika kwamba ni shida kuitawala nchi hiyo kubwa mfano wa eneo zima la Ulaya ya magharibi. Majadiliano lazima yafanyike ili kusaka ufumbuzi wa kudumu. Katiba mpya, madaraka kuenezwa majimboni badala ya kutuwama mahala pamoja hadi kufikia kubuniwa mfumo wa shirikisho, pakiwepo mabunge ya kimkoa, ni hatua nyengine muhimu. Wakati ambapo wengi ni vijana hawataki chochote chengine isipokuwa amani.

Mwandishi: Andrea Schmidt/Hamidou Oummilkheir
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman